IBRAHIMOVIC MWANASOKA BORA UFARANSA MARA YA PILI MFULULIZO
+5
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/ibrahimovic-mwanasoka-bora-ufaransa.html
Anajiuma uma: Ibrahimovic akijitahidi kuzungumza Kifaransa wakati wa kutoa hotuba ya kushukuru
MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1 kwa mara ya pili mfululizo.
Ibrahimovic
amefunga mabao 25 katika ligi na kuiwezesha PSG kutwaa taji la ligi
hiyo ya Ufaransa kwa rekodi ya kufikisha pointi 86 points, sambamba na
kufunga mabao 10 katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Na
Msweden huyo anayezungumza kwa ufasaha lugha tano tofauti za kimataifa,
aliwavunja mbavu wachezaji wenzake kwa kuzungumza Kifaransa kibovu.
Wakati
anazungumza, wachezaji wenzake wa PSG Salvatore Sirigu na Marco
Verratti walivunjika mbavu kwa kucheza Kifaransa chake kibovu.
Lakini
alipozungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Ibrahimovic alisema:
"Najivunia sana. Inaonyesha kwamba ulikuwa msimu mzuri kwa PSG. Kwangu, pia, labda bora zaidi katika maisha yangu ya soka,".
Mshindi mkuu: Ibrahimovic akiwa na tuzo zake
Ibrahimovic pia ameshinda Tuzo ya Bao Bora la Mwaka alilofunga katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Bastia Oktoba mwaka jana.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 32 pia amewahi kushinda ubingwa wa Uholanzi
mara mbili akiwa na Ajax (mwaka 2002 na 2004), Italia maarufu kama Serie
A akiwa na Inter Milan mara tatu ( kuanzia 2007 hadj 2009), La Liga
akiwa Barcelona (mwaka 2010), na Italia tena akiwa AC Milan (mwaka
2011).
Pia
alishinda mfululizo mataji ya Serie A akiwa na Juventus mwaka 2005 na
2006, lakini mataji hayo walipokonywa kwa kashfa ya cupping matokeo.
Ibrahimovic
atacheza mechi take ya mwisho msimu huu Jumamosi wakati PSG
itakapomenyana na Montepllier katika mechi za kufunga msimu na kwa
bahati mbaya hatakwenda Brazil kwenye Kombe la Dunia, kA kuwa Sweden
haijafuzu.