GIGGS KUPATA SHAVU MAN UNITED, VAN GAAL ASEMA HUWA ANABAKISHA KOCHA MMOJA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/giggs-kupata-shavu-man-united-van-gaal.html
Giggs akiwa benchi kwenye mechi dhidi ya Southampton, wengine ni wasaidizi wake Nicky Butt, Paul Scholes na Phil Neville
Tabasamu kubwa: Ryan Giggs anaweza kubakishwa kwenye benchi la ufundi msimu ujao
RYAN Giggs anaweza kupata kazi ya kudumu Manchester United baada ya kocha anayetarajia kujiunga na Mashetani wekundu, Louis Van Gaal kuweka wazi kuwa huwa anapenda kumuacha kocha mmoja aliyekuwa katika kikosi chake kipya kabla ya kujiunga na kuanza kazi rasmi.
Giggs alishuhudia timu yake ikimaliza mechi ya mwisho kwa sare ya 1-1 na Southampton jana.
Sasa kinachosubiriwa ni kuona nini Van
Gaal ataamua kuhusu hatima ya Giggs mara atakapothibitishwa kuwa kocha
wa United baadaye wiki hii.
Lakini
kutokana na falsafa ya Mholanzi huyo kubakisha moja ya makocha
waliokuwepo imetoa matumaini kwa Giggs kupata ajira ya kudumu.