ANGALIA PICHA YA MCHUNGAJI WA TANZANIA ANAYELINDWA KAMA RAIS
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/angalia-picha-ya-mchungaji-wa-tanzania.html
Maisha
ya Askofu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako, Geor Davie anayevuma zaidi
jijini Arusha na Dar es Salaam ni ya kifahari, anaabudiwa zaidi ya
manabii na analindwa kuliko marais mbalimbali duniani.
Davie
ambaye hujulikana zaidi kwa jina la Mtume, ana msafara mrefu kwenye
ziara zake anazokwenda kutoa huduma ambao husheheni magari mengi ya
kifahari kuliko marais wengi.
OneloveTz
tuna mlolongo wa matukio ya Davie ambayo yanajieleza kwa picha ambazo
zinabainisha namna mtumishi huyo wa Mungu anavyokula bata.
MSAFARA WA SHS. MIL. 200
Matukio yanaonesha kuwa, baadhi ya misafara ya Davie imekuwa na msururu mrefu wa magari ambayo hayapungui kumi.
Uchunguzi
umeonesha kuwa, magari hayo, kila moja linanunuliwa kati ya shilingi
milioni 20 na 40, hivyo thamani ya ‘mikoko’ peke yake inaleta wastani wa
jumla ya zaidi ya shilingi milioni 200 bila ya mafuta ambayo nayo
hugharimu fedha nyingi.
ULINZI DAH!
Kila
sehemu ambayo Davie hufika kwa lengo la kutoa huduma, huzungukwa na
walinzi kati ya nane na 10 ambao huvaa nadhifu, suti nyeusi na miwani
nyeusi.
Walinzi hao, humzunguka Davie na kufanya anapotembea asikaribiwe na watu kwa urahisi, huku wakimuongoza hatua kwa hatua.
Habari
zinadai kuwa walinzi hao wameajiriwa na Kanisa la Huduma ya Ngurumo ya
Upako na hulipwa mishahara kwa ajili ya kumlinda kiongozi huyo.
GARI LAKE LINA BENDERA MBILI
gari la Davie ambalo hupambwa na bendera mbili kama ilivyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa kawaida, gari la rais hupambwa na bendera mbili, moja ikiwa ya taifa na nyingine ya rais.
Hata
hivyo, blog hii halijapata ufafanuzi kuhusu bendera mbili za gari la
Davie, ingawa waumini wake wanasema kwamba ni alama ya huduma ya kanisa
lake.
NI RED CARPET KILA ANAPOKWENDA
Davie
anaheshimiwa kwa kiasi kikubwa na waumini wa huduma ya kanisa lake,
hivyo hutandikiwa zulia jekundu ‘red carpet’ kila anapokwenda kutoa
neno, huku akizungukwa na walinzi wake.
FULL KUABUDIWA
Neno la
Davie siyo tu kwamba linampa wafuasi bali pia kwa wengine humuabudu kwa
imani kuwa amejaliwa ufunuo mkubwa wa matatizo ya binadamu aliopewa na
Mwenyezi Mungu.
blog hili
lina picha za watu wakisujudu na kumshika viatu kwa imani kwamba tendo
hilo huwapa utakaso wa kiroho na matatizo mbalimbali.