ANGALIA PICHA MCHAWI ALIPONASWA KANISANI ARUSHA
Shabani akiwa na vitenda kazi vyake akiwa eneo la kanisa . Angalia picha za mtu aliyejitambulisha kwa jina la Shabani Hamisi alikuw...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/angalia-picha-mchawi-aliponaswa.html
Akiwa amevua shati huku akiwa anaombewa. |
Vitenda kazi vyake vikiwa vimemwagwa chini. |
Kazi kwelikweli. |
Alikosea njia meeen, akakutana na Yesu meen. Picha kwa hisani ya Ufufuo Crew. |
Katika hali
isiyo ya kawaida mtu huyu ajulikanaye kwa jina la Shabani Hamis amenaswa
akiwa anafanya uchawi katika kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha.
Matukio
ya kunaswa wachawi yamekuwa mengi kanisani hapo kutokana na uweza wa
Mungu unaojidhihirisha kupitia Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Frank
Andrew.
Pamoja, na kukutwa bila nguo mtu huyo aliyekuwa amebeba vifaa ambavyo
kwa mujibu wa maelezo yake, huvitumia kuwanga na kupaa ni pamoja na
tunguli na kikapo cha mkoba wa uchawi. Tukio hilo la aina yake limetokea
Usiku wa saa sita, wakati mkesha wa maombi ukiendelea kanisani hapo.
Baada ya maombi makali ya kuharibu uchawi katika anga la Arusha,
ikafuatiwa na tukio hilo. Mungu ni mkuuu maana hapana uchawi wala Uganga
juu ya watu wa Mungu.
Information Ministry - Arusha