Hamad Rashid aikosoa Tume ya Jaji Warioba
https://samchardtz.blogspot.com/2014/04/hamad-rashid-aikosoa-tume-ya-jaji.html
Mjumbe wa Bunge la Katiba,Hamad Rashid Mohammed
Tume
ya Mabadiliko ya Katiba, imevunja sheria kwa kupendekeza muundo wa
Muungano wa serikali tatu kwani haikupata theluthi mbili za Wazanzibari
na Watanzania Bara.
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Hamad Rashid
Mohammed, aliyasema hayo jana na kuikosoa Tume kuwa Wazanzibari walitaka
serikali ya mkataba siyo serikali tatu kama ilivyoeleza.
“Tume ilipata wapi mamlaka ya kusema Zanzibar inataka serikali tatu, walikaa nao wapi wakazungumza?," Alihoji.
“Ukichukua katiba na sheria ya
mabadiliko ya Katiba iliyopitishwa na Bunge inasema ili kufanya badiliko
la katiba ni lazima ipatikane theluthi mbili ya kura kwa Zanzibar na
Tanzania Bara.”
Mohammed ambaye alivuliwa wadhifa na
kufukuzwa uanachama wa CUF, alisisitiza kuwa kama Tume ya Warioba,
haikupata theluthi mbili hizo imevunja sheria.
“Kwa kuwa Tume yenyewe ndiyo
iliyoanza kuvunja sheria hiyo kwa sasa haina uhalali wowote hivyo
wajumbe kutoka Tanzania Bara waliopo wakae wapate theluthi mbili na sisi
kutoka Zanzibar tukae na kutengeneza theluthi mbili ili tupate Katiba
mpya,” alishauri.
Akizungumzia serikali mbili, alisema ndizo mwafaka kwani tatu zitaongeza gharama zaidi.
Alisema Tume ya Warioba haikukokotoa namna ya kuwatunza viongozi wakuu wakiwa madarakani na wanapostaafu.
“Leo Rais akisafiri anatumia si chini
ya Shilingi milioni 500, wakati mwingine hata bilioni moja,” alisema na
kuongeza kuwa hizo ni gharama wakiwa madarakani na wakistaafu
itakuwaje?
Alisema viongozi hao wakistaafu zaidi ya watatu kwa wakati mmoja utakuwa mzigo mkubwa wanabebeshwa wananchi.
“Tume haikuangalia gharama za miaka mingi ijayo,itakuwa gharama kubwa na kuhoji ni nani atazibeba?”