KENYA: MWENYE GARI LILILOLIPULIWA PANGANI ASHTAKIWA
WASHUKIWA watatu wa ugaidi miongoni mwao mwenye gari lililolipuka katika kituo cha polisi cha Pangani na kusababisha vifo vya watu w...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/04/kenya-mwenye-gari-lililolipuliwa.html
WASHUKIWA watatu wa ugaidi miongoni mwao mwenye gari lililolipuka katika kituo cha polisi cha Pangani na kusababisha vifo vya watu wanne miongoni mwao maafisa wawili wa polisi walifikishwa mahakamani Ijumaa.
Washukiwa
(kutoka kushoto), Mohamed Abdullahi Falir, Abdiaziz Bulle Ali na Ahmed
Dugali Ali wakiwa kortini Nairobi Aprili 25, 2014. Picha/PAUL WAWERU
Hata
hivyo hakuna mashtaka yoyote yaliyowasilishwa dhidi ya washukiwa hao ila
mahakama iliombwa iwazuilie kwa muda wa siku 10 katika kituo cha polisi
cha Muthaiga kusaidia polisi kukamilisha uchunguzi na mahojiano muhimu.
“Washukiwa
hawa ni hatari kwa usalama wa kitaifa na maslaha ya umma. Wandani wao
bado hawajatiwa nguvuni na wanasakwa na maafisa wa usalama kwa udi na
ufumba,”mahakama ilielezwa.
Mabw
Ahmed Dugal Ali (mwenye gari lililolipuliwa) , Abdiaziz Bule Ali na
Mohammed Abdullahi Falir waliofikishwa mbele ya hakimu mwandamizi Bi Eda
Agade chini ya ulinzi mkali katika Mahakama ya Milimani Nairobi
hawakutakiwa kujibu mashtaka.
Maafisa
wa kitengo cha polisi wa kupambana na ugaidi (ATPU) walisema kwamba
wanaume hao wanashukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Al
Shabaab.
Afisa
anayechunguza kesi hiyo Bw Cyrus Ikade, alisema katika taarifa aliyoapa
na kuwasilisha kortini kuwa washukiwa hao walitiwa nguvuni Aprili 24
kufuatia mlipuko huo ulioshtua wengi.
“Mshukiwa
wa kwanza (Ahmed Dugal Ali) ndiye mwenye gari ambapo maafisa hao wawili
wa polisi na magaidi wawili walifia,” anasema Bw Ikade na kuongeza, “
Mabw Abdiaziz Bulle Ali na Mohammed Abdullahi Falir wanashukiwa kuwa
wandani wa magaidi hao wa Al Shabaab walioangamia katika mlipuko huo.”
Nasaba
Bw Ikade
anasema kwamba alimtia nguvuni Bw Ali alipofika katika kituo cha Pangani
punde tu mlipuko huo ulipotangazwa na vyombo vya habari na “ kudai
ndiye mwenye gari hilo.”
Afisa
huyo wa polisi anasema kwamba washukiwa hao wote ni jamaa wamoja na
kwamba Abdullahi alishinda siku nzima na magaidi hao kabla ya mlipuko
huo kutokea jioni.
Dugal
amekana kwamba alikuwa na uhusiano wowote na magaidi hao na kwamba “
yuko tayari kuwasaidia maafisa wa polisi na taarifa yoyote wanayotaka.”
“Naomba
hii mahakama ifahamu ninalaani kitendo hivho cha ulipuaji maafisa wa
polisi katika kituo cha polisi cha Pangani. Niko tayari kuwasaidi
maafisa wa usalama na chochote watakacho,” alisema mahakamani Ijumaa.
Bi Agade
alifahamishwa polisi watafanya uchunguzi utakaosambaa hadi Mandera
ambapo uraia wao utathibitishwa. Pia polisi watafanya mahojiano zaidi.
Aliomba mahakama iwazuie kwa muda wa siku 10 ndipo uchunguzi ukamilishwe.
Afisa huyo anasema washukiwa hao wanatuhumiwa wanashirikiana na magaidi wanaotekeleza mashambulizi.
Bi Agade alikubalia ombi la maafisa wanaochunguza kesi hiyo na kuamuru washtakiwa wazuiliwe kwa muda wa siku 10.
Hakimu alifahamishwa washtakiwa hao walifikishwa kortini kabla ya masaa 24 kukamilika.