Flatnews

Urais UKAWA:Chadema yafuta mkutano wake Mbeya

Dk Slaa, Prof. Ibrahim .Lipumba. Chama cha Demokrasia na Maendeleo ...


Dk Slaa, Prof. Ibrahim .Lipumba.
Dk Slaa, Prof. Ibrahim .Lipumba.



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimea ahirisha  mkutano wake ulipangwa kufanyika jijini Mbeya  leo.Mkutano huo ulikuwa ni katika  ziara ya Dk Slaa ambapo ilipangwa awahutubie wananchi katika jiji hilo.

Kwa mujibu wa Mratibu wa chama hicho Kanda ya Nyasa (Chadema), Frank Mwaisumbe amesema sababu ya kufutwa ni viongozi wa kitaifa kuendelea na vikao vya ngazi ya juu jijini Dar es Salaam.
Hata  hivyo Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Joseph China alisema ziara hiyo imefutwa kutokana na viongozi wakuu wa kitaifa kutingwa na vikao vya Ukawa.
Viongozi wa kitaifa wa Chadema wakiwa Mwanza walitangaza kwamba wangefanya mikutano mingine, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam.
Vyanzo mbalimbali kutoka ndani ya umoja wa Ukawa vinadai kwamba  umoja huo uko bize na mchakato wa kumpata mgombea wake wa Urais anayedaiwa kuwa atatangazwa rasmi agosti 4 mwaka 2015.
Kitendawili katika umoja huo ni kwamba nani atapeperusha bendera ya umoja huo kufuatia kuwepo madai ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kuwa na Mpango wa kuhamia UKAWA hususani chama cha Chadema lakini hata hivyo taarifa hizo hakuna aliyeweza kuzithibitisha huku michakato ime endelea kuwa siri nzito.

Related

NEWS 6958193836962653253

Post a Comment

emo-but-icon

item