Kajala afungukia kuingia kwenye siasa
Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amefungukia kuingia kwenye siasa kuwa ni bora abaki ...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/kajala-afungukia-kuingia-kwenye-siasa.html
Staa
wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amefungukia kuingia kwenye
siasa kuwa ni bora abaki kwenye upenzi na chama fulani kwani hawezi
kugombea.
Akizungumza
juzikati, Kajala alisema kuwa, japokuwa wasanii wengi wakiwemo wa
tasnia ya filamu Bongo, wamekuwa wakichukua fomu za kutaka kugombea
nafasi mbalimbali za udiwani na ubunge lakini kwake hafikirii kitu kama
hicho.
“Mimi
siasa siiwezi kabisa, kifupi haipo kwenye damu ndiyo maana unaona
wenzangu wote wamechukua fomu za kugombea mimi wala sijajitokeza
kuchukua,” alisema Kajala.