KUJUCHUKULIA SHERIA MKONONI BADO NI TATIZO TANZANIA,REPORT YA LHRC YAIBUKA NA MENGI,ISOME HAPA
Moja kati ya matukio ya kujichukulia sheria mkononi yaliyowahi kutokea nchini.
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/kujuchukulia-sheria-mkononi-bado-ni.html
![]() |
| Moja kati ya matukio ya kujichukulia sheria mkononi yaliyowahi kutokea nchini. |
Kituo cha sheria na
haki za binadamu Tanzania LHRC leo wametoa Report ya Haki za binadamu kwa
kipindi cha nusu mwaka huu wa 2015 report ambayo inaonyesha ukiukwaji mkubwa wa
haki za binadamu katika Nyanja mbalimbali.
Taarifa hiyo ambayo ni
matokeo ya Tafiti mbalimbali zilizofanywa na kituo cha sheria na haki za
binadamu LHRC inaonyesha kuwa swala la haki ya kuishi kwa watanzania bado
imeendelea kukiukwa ambapo katika utafiti huo unaonyesha kuwa kwa kipindi cha
nusu mwaka pekee watu takribani 366 waliuawa kutokana na raia kujichukulia
sheria mkononi jambo ambalo limetajwa kuangamiza maisha ya watanzania walio
wengi.
| Mtafiti kutoka kituo hicho ndugu PAUL MIKONGOTI akizngumza na wanahabari wakati akitoa ufafanuzi wa Report hiyo leo Jijini Dar es salaam |
Akitoa ufafanuzi juu ya Report hiyo mtafiti kutoka kituo hicho ndugu PAUL MIKONGOTI amesema kuwa
matatizo ya kujichukulia sheria mkononi yamekuwa yakiwahusisha zaidi watu
wanaokuwa na tuhuma za wizi,na hasa vibaka,huku akisema kuwa matukio mengi ya
kujichukulia sheria mikononi yamekuwa hayatolewi taarifa kwenye vyombo vya habari
hasa matukio yanayotokea vijijini.
Mauaji mengine ambayo
yamejitokeza katika report hiyo ni mauaji ya askari hasa wawapo kazini,ambapo
kwa kipindi hiki cha nusu mwaka vituo vinne vilivamiwa na kusababisha vifo
vya askari watatu jambo ambalo limeendelea kugarimu maisha ya askari hao.
| Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA akifafanua jambo |
Tofauti na haki ya
kuisha ambayo imejitokezaa katika Report hiyo iliyotolewa leo haki nyingine
ambazo zimeonekana kukiukwa kwa hali ya juu ni pamoja na haki za wanawake na
watoto,haki ya bkiupata habari na uhuru wa habari,haki ya afya bora,haki ya
kupiga kura,pamoja na maswala ya rushwa na utawala bora yamejitokeza sana
katika report hiyo.
Akizungumzia Report hiyo
mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bi HELLEN KIJO
BISIMBA amesema kuwa swala la kujichukulia sheria mkononi limezidi kuwa kubwa
na imefika kipindi sasa kwa watuhumiwa wa kuchukua sheria mkononi na wale wa
mauaji yatokanayo na imani za kishirikina washughulikiwe kama wahalifu wengine
kwa mujibu wa sheria za nchi jambo ambalo linaweza nkupunguza hali hiyo
Aidha ameishauri
serikali kuhakikisha kuwa inarekebisha mfumo wa utoaji wa haki unaboreshwa ili kutopa
haki kwa wote huku ikiendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kurekebisha
mkifumo hiyo.
Taarifa iliyotolewa leo
imejikita zaidi katika maeneo machache ya haki za binadamu ambayo yameoinyesha
kuwa na ukiukwaji wa hali ya juu katika kipindi cha nusu mwaka ambapo taarifa
kamili ya hali ya haki za binadamu nchini itaandaliwa mwishoni mwa mwaka.
UKITAKA KUSOMA TAMKO NZIMA LIPO CHINI HAPO
