Chris Brown kwenye headlines, azuiliwa kuondoka Ufilipino mpaka alipe…!!
Chris Brown anaziandika headlines kwa mara nyingine tena, siku chache zilizopita staa huyu alikuwa Ufilipino kwa ajili ya kufanya show...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/chris-brown-kwenye-headlines-azuiliwa.html

Chris Brown anaziandika headlines kwa mara
nyingine tena, siku chache zilizopita staa huyu
alikuwa Ufilipino kwa ajili ya kufanya show, lakini
akazuiliwa kuondoka nchini humo jana kutokana
na mzozo wa mkataba wake wa nyuma.
Chris Brown alizuiliwa Airport siku ya Jumatano
asubuhi akiwa anajiandaa kuondoka na ndege
yake binafsi kutoka Manila International Airport
kwenda Hong Kong kwa ajili ya concert nyingine.

Chombo cha Sheria na Haki Ufilipino ilitoa amri
siku ya Jumanne usiku kumzuia Chris Brown
kuondoka nchini humo mpaka atakapolipa hela za
Promoters walioandaa show kipindi cha mwaka
mpya, show ambayo Chris hakutokea.

Kwa sasa Chris Brown ameambiwa kama atahitaji
kuondoka nchini humo kwa sababu za msingi
basi itambidi aombe ruhusa kwa Ofisi ya Uhamiaji
ambao kama wakikubali basi watampatia cheti
kinachoonyesha sababu hizo ni za mzingi na
kuwa atarudi.