Je Di Maria anaondoka Man Utd, kituo cha TV cha mmiliki wa PSG kina majibu haya..
siku kadhaa baadhi ya vyombo vya habari nchini Ufaransa vimekuwa vikiripoti kwamba mchezaji huyo angeuzwa kwa ada ya zaidi ya Eu...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/je-di-maria-anaondoka-man-utd-kituo-cha.html

siku kadhaa baadhi ya vyombo vya habari nchini
Ufaransa vimekuwa vikiripoti kwamba mchezaji
huyo angeuzwa kwa ada ya zaidi ya Euro Millioni
60 na angetambulishwa rasmi na PSG Ijumaa hii,
lakini kwa mujibu wa kituo cha Televisheni cha
BeIN Sports kinachomilikiwa na bwana Nasser
Ghanim Al-Khelaifi, ambaye mmiliki wa klabu ya
PSG – ni kwamba klabu hiyo imeghairi kumsajili
mchezaji huyo na mazungumzo baina ya United
na PSG yameisha

Akiwa na miaka 27, Manchester United walivunja
rekodi ya usajili ya Uingereza kwa kulipa kiasi cha
£59.7m kumsajili Angel Di Maria lakini
muargentina huyo ameshindwa kuhimili
mikikimikiki ya ligi kuu ya EPL na inaaminika
anavutiwa na wazo la kwenda PSG.
Hata hivyo, inaonekana vilabu hivyo vimeshindwa
kuafikiana juu, huku CEO wa United akiripotiwa
kutaka kurudisha fedha zote walizotumia kumpata
winga huyo.