Uwanja wa Mashabiki: Saga la Ladie Vs Ricky Bahl Vs Mzee wa Swaga
Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki mitandaoni kuhusiana na SAGA la Ladies Vs Ricky Bahl Vs Mzee wa Swaga w...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/02/uwanja-wa-mashabiki-saga-la-ladie-vs.html
Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki mitandaoni kuhusiana na SAGA la Ladies Vs Ricky Bahl Vs Mzee wa Swaga walioziona zote mbili.
Inasikitisha sana kama wasanii wetu wanaweza kufanya uhuni huu na kutuaminisha watanzania kwamba wametunga wao.
Binafsi nimeangalia muvi ya Ladie Vs Ricky Bahl mwaka 2011 na ni moja kati ya movie ya kihindi niliyoipenda kutokana na maudhui yaliyo kwenye movie hiyo.
Ricky Bahl alicheza kama Conman mtaalam aliyekuwa anawalaghai wadada mbalimbali kwa mapenzi ya dhati kumbe alikuwa akiwaaminisha ili awatapeli na kweli alifanikiwa kufanya kwa wadada hao.
Alikuwa ana uwezo wa kubadilisha muonekano wake na ku-appear tofauti tofauti hivyo kuwa ngumu kumtambua.
Sasa huyu bwana mkubwa bonge la Bwana kaiba idea nzima nzima bila hata kufigha,nafikiri alidhani kwakuwa tokea hiyo muvi ya kihindi imetoka ni muda mrefu(2011) hivyo watu tutakuwa tumesahau, kumbe sio!!
Niliangalia vizuri Kipindi cha Zamaradi kwa jinsi alivyokuwa akielezea na nilistaajabu sana. Kuiba idea sio vibaya kama utaweka umma wazi kuwa ile movie umechukua idea na kuitengeneza katika maadhi ya Kibongo bongo.
Hata ukiangalia wahusika wakuu, kwenye muvi ya Kihindi walikuwa watano na hata ya JB watano pia ( Mwanaume mmoja na wadada Wanne).
Nisieleze mengi lakini jamaa kaiba kwa asilimia 99 na mbaya zaidi kaudanganya umma na mashabiki wake kwamba yeye ndio mtunzi wa muvi hiyo.
Wasanii tubadilike, Tunaitia Tanzania aibu.
Asanteni.
By Chachu Ombara
Nimeziona zote mbili, jamaa ka copy na kupaste yani ni vile vile, kule kuna msichana anaitwa Ishika Desai/ Patel ndiyo amesimama kama yule msichana ambaye JB kapenda na kumrudishia pesa zake mwishoni, katika hiyo movie ya kihindi kuna msichana anaitwa Raina huyu ktk mzee wa swaga nafasi yake imechukuliwa na yule dada anaongea sana kingereza aliyepewa dola bandia, kuna msichanana anaitwa Dimple katika mzee wa swaga nafasi yake imechukuliwa na Wastara, na mshiriki mkuu wa mwisho ni Thea ambapo katika ile ya kihindi thea amechukua nafasi ya mdada anaitwa Saira, yani kacopy pale pale Duh
By Gody Godwin Unstoppablé Arsenal
Swali je kucopy bila kutoa credit kwa uliyemcopy ni wizi au ujanja/kipaji??
