Wayne Rooney ‘ hakunaga’ England, akiri alitaka Ronaldo atolewe katika mchezo wa England v Ureno, 2006
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/wayne-rooney-hakunaga-england-akiri.html

Nahodha wa England, Wayne Rooney alifunga bao la mkwaju wa penalti na kumfanya kushika nafasi ya 3 katika listi ya wafungaji bora wa muda wote wa ‘ The three lions’. England ilishinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Slovenia, jana Jumamosi katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za ulaya, 2016, Ufaransa. Siku moja kabla ya mshambulizi huyo wa klabu ya Manchester United kucheza mchezo wake wa 100 wa kimataifa alikiri kujaribu kufanya njia za udanganyifu ili Cristiano Ronaldo atolewe nje wakati wa mchezo wa robo fainali wa kombe la dunia, 2006, Ujerumani.
Katika mchezo huo, Rooney ndiye aliyekuja kuondoshwa uwanjani kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya, mlinzi wa Ureno, Ricky Carvalho. Ronaldo ambaye alichukiwa sana na mashabiki wa kandanda wa England kutokana na shinikizo aliloweka ambalo lilichangi kuhakikisha Rooney anatolewa nje na mwamuzi, Horacio Elizondo.
” Naelewa kwa nini alishinikiza nipewe kadi. Alifanya hivyo kuhakikisha Ureno inashinda” anasema, Rooney kuhusu tukio hilo lililotokea miaka nane iliyopita.
“Niwe muungwana tu, hata mimi nilitenda kama hivyo kuhakikisha Ronaldo anatolewa uwanjani kwa maslahi ya England. Ndiyo, nilitaka kuhakikisha anatolewa nje ya uwanja, huo ni ukweli mtupu” aliongeza kusema mchezaji huyo mwenye mabao 50 katika michezo 100 ya England. ” Katika kipindi cha kwanza, nilimwambia mwamuzi amuadhibu Ronaldo kwa kumpa kadi ya njao, kwani alikuwa anajirusha mno.”.
Baada ya tukio hilo ilifikiriwa wachezaji hao wasingeweza kufanya kazi kwa pamoja, lakini waliweza kushirikiana kuinyanyua Manchester United na kushinda mataji matatu mfululizo ya ligi kuu, taji moja la mabingwa ulaya, klabu bingwa ya dunia na vikombe lukuki vya ndani ya England chini ya Sir Alex Ferguson, kocha ambaye aliwatuliza wachezaji hao walikuwa makinda na kucheza kwa uelewano mkubwa.
“Hiki ni kitu cha kawaida katika soka, kwani wachezaji mara nyingi wanazungumza na mwamuzi ili kumshawishi jambo fulani. Mara baada ya mechi nilizungumza na Ronaldo moja kwa moja”