TUNAHITAJI MIAKA MIA SITA KUTOKEA KWA MESSI MWINGINE
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/tunahitaji-miaka-mia-sita-kutokea-kwa.html

Lionel Messi amejiweka kwenye ulimwengu wa magwiji baada ya usiku wa jumanne kufunga matatu yalioiwezesha Barcelona kushinda mabao manne kwa sifuri mbele ya Apoel, na sasa Lionel Messi anakuwa mshambuliaji wa wakati wote wa ligi ya mabingwa akifikisha mabao 74, mabao manne mbele ya Cristiano Ronaldo matatu mbele ya aliyekuwa anashikilia rekodi hiyo Raul Gonzalez.
Rekodi anazoweka Messi zinamfanya ajiweke kwenye daraja moja na magwiji wa soka waliowahi kutamba kwenye sayari hii ya ulimwengu kama Pele pamoja na Diego Armando Maradona kutokana mafanikio yake makubwa aliyoyapata kwenye ngazi ya klabu kitu kinachomtofautisha Messi na magwiji hao ni mafanikio makubwa waliopata magwiji hao kwenye ngazi ya kimataifa likiwemo taji la kombe la dunia.
Mwishoni mwa juma lililopita Lionel Messi alivunja rekodi ya kuwa mfungaji wa wakati wote wa ligi kuu Hispania baada ya kuvunja rekodi ya Telmo Zarra ya mabao 251, mwishoni mwa mwa juma lililopita Messi alifunga hatric na kufikisha mabao 253.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Argentina mpaka sasa amefunga mabao 368 kwenye kipindi cha miaka 11 alichoichezea Fc Barcelona.

Rekodi nyingine za Messi ni mfungaji aliefunga magoli mengi kwenye msimu mmoja mabao 68.
Aidha Messi anashikilia rekodi ya kutwaa mara nne tuzo ya Ballon d’Or .
Mshambuliaji bora mara nne barani Ulaya akiwa sawa na gwiji Gerd Muller.
Mshambuliaji aliyepiga hatric nane kwenye msimu mmoja wa La Liga .
Pia Lionel Messi anashikilia rekodi ya kufunga mabao 91 ndani ya mwaka mmoja.
Lione Messi anashikilia rekodi ya kufunga mabao 50 kwenye msimu mmoja wa ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga.
Kubwa zaidi Messi anajivunia rekodi ya kufunga magoli katika michezo 21 mfululizo ya La Liga .
Aidha Messi maarufu kama la pulga anashikilia rekodi ya kufunga mabao matano kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kwenye rekodi anaungana na mshambuliaji wa Shaktar Donesk Luiz Adriano.
Kama haitoshi nyota huyo wa kimataifa wa Argentina ndio mshambuliaji aliefunga mabao mengi kwenye Clasicos amefunga mabao 21.
Pia ndio mshambuliaji mwenye mabao mengi kwenye klabu bingwa ya dunia amefunga mabao manne sawa na Denilson.