Flatnews

FAINALI YA MANCHESTER CITY IKO ROME, DESEMBA 10, ESTADIO OLIMPIC


man 1
Manchester City imefufua matumaini ya kufuzu kwa hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya kuishinda Bayern Munich kwa mabao 3-2 katika dimba la Etihad usiku wa kuamkia leo. Mabingwa hao wa England bado wanaburuza mkia wa kundi wakiwa na alama tano sawa na AS Roma walio katika nafasi ya pili na CSKA Moscow walio katika nafasi ya tatu. Munich tayari wamefuzu kwa hatua ya mtoano licha ya kukutana na kipigo hicho.

Roma chini ya kocha, Rud Garcia wanaweza kufuzu kwa hatua inayofuata kama washindi wa pili wa kundi endapo wataishinda City katika mchezo wa mwisho mapema mwezi ujao katika uwanja wa Olimpiki, Rome. Fransisco Totti, mshambulizi mwenye miaka 38 ambaye aliamua kutostaafu soka baada ya Roma kurudi katika michuano ya ulaya alifunga bao lake la tatu msimu huu katika michuano hiyo, lakin I halikutosha kuwapa pointi tatu jijini Moscow na kujikuta waliondoka na pointi moja baada ya wenyeji kusawazisha kupitia kwa Vasily Berezutskiy dakika ya mwisho ya mchezo.
Roma na CSKA zote zimefungana kwa kila kitu. Munich watacheza na Warusi hao katika dimba la Allianz Arena, Disemba 10, siku ambayo pia Roma na City zitakuwa zikipambana. Kocha wa City, Mchile, Manuel Pellegrini amesema kuwa mshambulizi wake Sergio Aguero ataendelea kufanya vizuri msimu huu, Muargentina huyo alifunga mabao yote matatu katika ushindi dhidi ya Munich hali ambayo imempa matumaini kocha wake ambaye anaamini watafuzu mbele ya Roma .
Kevin Strotman aliingia uwanjani na kucheza kwa mara ya kwanza baada ya miezi sita, kiungo huyo a,mbaye aliumia goti miezi sita iliyopita alicheza kwa dakika saba za mwish baada ya kuchukua nafasi ya Mbelgiji, Radja Nainggolan. Miralem Pjanic, Yao Gervinho, Seydou Keita, Danielle de Rossi, Ashley Cole ni baadhi ya wachezaji mashuhuri ambao hawatapenda kuona timu yao ikiondolewa katika uwanja wa nyumbani.
Mchezo kat ya Roma na City ni kama fainali lakini unaweza kuwapa nafasi ya kufuzu CSKA kama timu hizo zitashindwa kufungana na Warusi hao wakaifunga Munich. Kabla ya mchezo dhidi ya Munich, kiungo wa City, Samir Nasri alisema kuwa endapo timu hiyo itashindwa kufuzu kwa hatua ya mtoano nyota wengi watakutwa na fagio klabuni hapo.
Dakika tano za mwisho ziliweza kuwasaidia nyota hao wa gharama kupumua walau kwa muda. City imepambana sana dhidi ya Munich, lakini haitoshi, watatakiwa kwenda ‘ Mji Mtakatifu’ na kumuangusha ‘ King of Roma’ ambaye alikacha kustaafu soka ili kucheza michuano ya mabingwa ulaya.

Post a Comment

emo-but-icon

item