TAZAMA PICHA ZA MTU MREFU ZAIDI NA MTU MFUPI ZAIDI DUNIANI WALIPOKUTANA KWA MARA YA KWANZA
Tumekuwa tukisikia rekodi mbalimbali zikivunjwa na watu duniani na rekodi hizo maalumu huwa zinatunzwa katika kitabu cha kumbukumb...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/tazama-picha-za-mtu-mrefu-zaidi-na-mtu.html

Tumekuwa
tukisikia rekodi mbalimbali zikivunjwa na watu duniani na rekodi hizo
maalumu huwa zinatunzwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Guiness World
Records.
Kwa
mara ya kwanza, watu ambao wako katika kitabu hicho kutokana na kuvunja
rekodi hizo za kipekee wamekutana London Uingereza siku ya Novemba 13.
Chandra Bahadur Dangi mtu aliyevunja rekodi ya kuwa mtu mfupi kuliko wote Duniani amekutana kwa mara ya kwanza na Sultan Kosen, jamaa ambaye amevunja rekodi ya kuwa mtu mrefu zaidi duniani.
Chandra anatokea Nepal ana urefu cha Sm. 54.6, Sultan anatokea Uturuki ana urefu wa Sm. 251 ambayo ni sawa na futi 8.3.
Hizi ni picha zinazowaonyesha wakali hao wakiwa pamoja.



