GUMZO AIRPORT! DIAMOND AJIFUNGIA KWENYE GARI KUKWEPA MAPAPARAZI AKIMSINDIKIZA ZARI 'THE BOSS LADY'
BAADA ya kula bata za kutosha Bongo, wakati wakisindikizana kimahaba, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mr...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/gumzo-airport-diamond-ajifungia-kwenye.html
BAADA ya
kula bata za kutosha Bongo, wakati wakisindikizana kimahaba, staa wa
Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mrembo mkali kutoka
Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, wamezua gumzo kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, Ijumaa lina
mchapo kamili.
Mrembo
mkali kutoka Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady (mwenye
gauni jekundu) akishuka kutoka gari la ‘Diamond Platnumz’.
HABARI KAMILI
Tukio
hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri mishale ya mchana,
Jumanne iliyopita katika maegesho ya airport (uwanja wa ndege) ambapo
Diamond alikuwa akimsindikiza Zari aliyekuwa akitimua Bongo baada ya
kufanya yao kwa siku kadhaa.
KABLA YA TUKIO
Awali
kabla ya tukio hilo, gazeti hili lilipokea ‘ubuyu’ kutoka kwa chanzo
chake cha kuaminika kwamba, wawili hao walikuwa wakijiandaa katika
hoteli waliyokuwa kwa siku kadhaa iliyopo kwenye Ufukwe wa Bahari ya
Hindi, tayari kuelekea uwanja wa ndege.
Zari au The Boss Lady akimwelekeza kitu mpambe wa 'Diomond'.
“Ijumaa
acheni kulaza damu, kwa taarifa yenu Diamond ndiyo anajiandaa kumpeleka
Zari airport wahini pale mpate tukio kamili ili kumaliza ubishi kuwa
kweli walikuwa wote Bongo,” kilisema chanzo hicho kikiomba hifadhi ya
jina gazetini.
IJUMAA MZIGONI
Baada
ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walitia gia kwenye ‘motokaa’
ambapo dakika kadhaa baadaye walikuwa wametega satelaiti zao uwanjani
hapo tayari kwa kunasa tukio.
Gari
jeusi aina ya BMW X6 ya mkali 'Diamond' ikiendeshwa na mpambe
wake aliyejulikana kwa jina la Q-Boy huku mwenyewe (Diamond) siti ya
nyuma.
BMW X6 LATOKEA
Wakati
wanahabari wetu wakiwa wanakaribia kukata tamaa, ghafla lilitokea gari
jeusi aina ya BMW X6 ambalo tofauti na magari mengine, badala ya namba
za usajili, lenyewe lilikuwa na maandishi yaliyosomeka kwa herufi kubwa
‘PLATNUMZ’ kisha likapaki kwenye eneo la maegesho uwanjani hapo.
Gari
hilo lilikuwa likiendeshwa na kijana mmoja wa Diamond aliyejulikana kwa
jina la Q-Boy na pembeni mwake kwenye siti ya abiria alikuwepo mpambe
mwingine wa msanii huyo ambaye jina halikupatikana.
DIAMOND AJIFUNGIA
Wakiwa
siti ya nyuma, wakati Zari anashuka, Diamond alijifungia kwenye gari
ili kuwakwepa mapaparazi baada ya kuwashtukia kuwa walikuwa wakimsubiri.
Zari au The Boss Lady akisindikizwa na mpambe wa 'Diamond'.
WAZUA GUMZO
Wawili
hao walizua gumzo uwanjani hapo ambapo baadhi ya watu wakiwemo Wazungu
walikuwa wakiwashangaa huku Wabongo wakitamani Diamond atoke kwenye gari
amtambulishe Zari kama ndiye mrithi wa Wema au la!
“Huyu
Diamond naye balaa. Kampata wapi mtoto mrembo kiasi hiki? Hakyanani na
mimi bora niwe msanii nitafaidi. Mtoto kaumbika hasa,” alisikika mmoja
wa madereva teksi huku wenzake wakimkatisha tamaa kuwa hawezi kuwa
msanii. Zari alishuka na yule mpambe wa Diamond na kuambatana hadi
sehemu ya kukaguliwa ili akapande ndege.
Zari, 'The Boss Lady' akilonga jambo na paparazi wa gazeti la Ijumaa.
IJUMAA LAMBANA ZARI
Kabla
ya kufikia sehemu hiyo, wanahabari wetu walibahatika kumfotoa picha za
kutosha Zari kisha kumfuata na kumuuliza alikuwa na ishu gani na Diamond
ambaye alikuwa naye hotelini Bongo kwa takriban siku tano.
Hata
hivyo, Zari alishindwa kujibu na kuishia kusema kuwa hana maoni.“No
comment,” alisema Zari na hata alipoombwa kufafanuzi kidogo aligoma.
DIAMOND AFUNGUKA
Baada
ya tukio hilo, wanahabari wetu walimtafuta Diamond kwa njia ya simu ili
azungumzie kwa kina juu ya uwepo wa Zari Bongo na tuhuma za kujihusisha
naye kwenye mapenzi ambapo Diamond alifunguka:

Mbongo Fleva 'Diamond' wakati akitanua na Zari, 'The Boss Lady'.
“Niliwaona airport mkimpiga picha na gari langu na mkaongea naye.
“Kweli ninyi ni noma sana, lakini nadhani mliandika hivi karibuni kuwa mimi nimeachwa na Wema (Sepetu).
“Ukweli
hakuna mwanaume anayeweza kujitoa kwa demu wake hasa kumpatia zawadi ya
gari kama niliyotoa kwenye bethidei ya Wema halafu baadaye usikie kuna
mwanaume mwingine katoa zaidi na ukaendelea kufurahia.
ZARI NI RAFIKI TU JAMANI!
“Sitaki kuongea mengi ila Zari naomba atambulike kama rafiki yangu tu jamani.”
YATOKANAYO
Hivi
karibuni Diamond alimwagana na Wema ambapo siku chache baadaye habari
zilivuja kwamba Zari ambaye ni msanii wa kike tajiri Afrika Mashariki
ndiye mwenye uwezo wa kuziba pengo hilo mara tu baada kuonekana na jamaa huyo.Credit GPL