TAMKO LA SERIKALI KUHUSU WIZI UNAOFANYWA NA MAKUMPUNI YA SIMU TANZANIA KWA WATEJA WAO.
Watumiaji wengi wa huduma ya simu za mkononi wamekuwa wakilalamikia wizi wa pesa unaofanywa na baadhi ya makampuni hayo, jana ka...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/tamko-la-serikali-kuhusu-wizi.html
Watumiaji
wengi wa huduma ya simu za mkononi wamekuwa wakilalamikia wizi wa pesa
unaofanywa na baadhi ya makampuni hayo, jana katika kikao cha Bunge
Dodoma Serikali imesema inatambua kuhusu wizi unaofanywa na baadhi ya
makampuni ya simu za mkononi na kutoa tamko namna ambavyo imejipanga
kukabiliana na wizi wa aina hiyo.
Akitoa tamko hilo Naibu
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba alisema
Serikali itaanzisha kituo maalum cha kushughulikia malalamiko hayo CCC,
kitakachokuwa kinasimamiwa na TCRA.
Akiuliza swali kuhusiana na jinsi Serikali ilivyojipanga kukabiliana na wizi huo Mbunge wa Konde Khatib Said Haji alisema;
“Wizi
huu unaofanywa na makampuni ya simu si wizi mkubwa kama ule wa ESCROW..
ni wizi mdogo mdogo unaowaibia Watanzania elfu tano elfu tatu lakini
kwa ujumla wake, Mpemba aliyeko Konde akiibiwa elfu tatu, Mnyamwezi wa
Tabora elfu mbili, Ukizijumlisha ni mamilioni ya shilingi wanaibiwa
Watanzania… Leo watu hao elfu tatu elfu mbili unawaambia wapeleke
malalamiko yao, gharama hiyo umeikadiriaje hata mtu huyo akadai
malalamiko ya elfu tatu..”
“Hivi
serikali yenu makini imekuwa wapi muda wote mpaka kukiri kama
Watanzania wamekuwa wakiibiwa na bila wenyewe kujijua?, na bado hamna
hatua mlizozichukua, ni nani aliyeko nyuma ya pazia hili la kuibia
Watanzania na ninyi mkaridhia ama ni yale yaliyosemwa kama CCM ina fund
katika wizi huu..?”- Khatib Said Haji.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba alisema;
"Napenda
nikiri tatizo la wizi au dhuluma kwa wateja lipo na ndio lililopelekea
tukaweka hizi kanuni ambazo zinaweka adhabu na hatua za kuchukua katika
kudhibiti wizi huo.. Licha ya utaratibu wa kawaida wa kulalamika katika
makampuni ya simu, kwa sababu moja ya matakwa ya sheria ni kwamba
kampuni za simu zinapaswa kuweka utaratibu wa kuhudumia wateja wake,
lakini tumebaini kwamba utaratibu huo una matatizo, unaweza ukapiga simu
muda mrefu isipokelewe, unaweza kuambiwa usubiri na wakati unasubiri
kulalamika pia unakatwa..
"Kwa hiyo Serikali
inafahamu hilo, pamoja na hatua tulizozichukua ni kuweka ule mtambo wa
kufuatilia mawasiliano ambao moja ya kazi yake sio kufuatilia tu mapato
lakini ubora wa mawasiliano.. Kwa kutambua kuwa makampuni ya simu haya
wakati mwingine yanachelewa wakati mwigine yanapuuza wateja, kituo hiki
ambacho tunakianzisha namba zake zitasambazwa kila mtu atakuwa nayo, kwa
hiyo huna haja kusafiri kufuatilia shilingi elfu mbili elfu tatu elfu
tano. Kutakuwa na namba ambayo ni bure kupiga..”- January Makamba.
“ Kila
utakapopiga kulalamika utapewa namba maalum ya lalamiko lako, na
lisiposhughulikiwa hata kitengo cha kampuni ya simu kutoshughulikia
lalamiko lako na yenyewe itakuwa sababu ya makampuni hayo kuadhibiwa..”- January Makamba.
