DEWJI BILIONEA NAMBA MOJA TANZANIA, ROSTAM AZIZ ANAMFUATIA
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji (39), ametajwa kuwa ndiyo bilionea namba moja nchini kwa sasa, akifuatiwa na Rostam Aziz (4...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/dewji-bilionea-namba-moja-tanzania.html
Mfanyabiashara
maarufu nchini, Mohammed Dewji (39), ametajwa kuwa ndiyo bilionea namba
moja nchini kwa sasa, akifuatiwa na Rostam Aziz (49).

Kwa
mujibu wa ripoti ya Jarida la Ventures Afrika lililotolewa jana,
wafanyabiashara hao ndiyo Watanzania pekee waliongia kwenye orodha ya
mabilionea 55 barani Afrika.
Dewji,
ambaye pia ni mbunge wa Singida Mjini kwa tiketi ya CCM, ni
mfanyabishara kijana aliyekamata nafasi ya 24 katika orodha hiyo akiwa
na utajiri wa Dola 2 bilioni Marekani (Sh3 trilioni).
Nafasi hiyo inamfanya kijana huyo kutambulika kama tajiri namba moja nchini kwa sasa na siyo tena Rostam.
Katika
orodha hiyo Dewji amemwacha Rostam kwa nafasi 16. Rostam anashika
nafasi ya 40 akiwa na utajiri wa Dola 1.2 bilioni za Marekani.
Mwaka
jana, Rostam alitajwa kuwa ndiye tajiri namba moja Tanzania. Hiyo
ilikuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na jarida la Marekani la
Forbes. Rostam alikamata nafasi hiyo na ya 27 katika Afrika akiwa na
utajiri wa Dola 1 bilioni za Marekani (Sh1.6 trilioni).
Katika orodha hiyo, yumo pia Said Bakhresa ambaye aliwahi kutajwa siku za nyuma kuwa mmoja wa mabilionea wa Tanzania na Afrika.
Hata
hivyo, ripoti ya jarida hilo ya mwaka 2011, ilimtaja Bakhresa kuwa
ndiye aliyekuwa tajiri namba moja wa Tanzania. Bakhressa katika kipindi
hicho alikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 620 milioni (Sh971 bilioni)
akifuatiwa na Rostam, Mengi na mfanyabiashara mwingine maarufu, Ali
Mufuruki.
Mengi alishikilia nafasi ya pili Tanzania na 34 Afrika akiwa na utajiri wa Dola 550 za Marekani (Sh861 bilioni).
Forbes
ilionyesha kuwa Bakhresa alifungana na Mo katika nafasi ya tatu ya
orodha ya matajiri wa Tanzania na ya 38 kwa Afrika. Wote walikuwa na
utajiri wa Dola 500 milioni (Sh783 bilioni). Jarida hilo limemtaja pia
tajiri kijana wa Nigeria mwenye umri sawa na Dewji, Igho Sanomi kuwa
anashika nafasi ya 30 akimiliki Dola 1.3 bilioni.