SITTI MTEMVU BADO KITI CHA MOTO, MAMLAKA ZAJIPANGA KUMPELEKA MAHAKAMANI.
Uamuzi mgumu wa kujivua taji la Miss Tanzania 2014, haujamaliza misukosuko inayomkabili Sitti Mtemvu. Wakala wa Uzazi, Vifo na...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/sitti-mtemvu-bado-kiti-cha-moto-mamlaka.html
Uamuzi
mgumu wa kujivua taji la Miss Tanzania 2014, haujamaliza misukosuko
inayomkabili Sitti Mtemvu. Wakala wa Uzazi, Vifo na Ufilisi (Rita)
wamedai kuwa wamekamilisha upekuzi wa taarifa alizotumia kuombea cheti
cha kuzaliwa na vielelezo hivyo vimepelekwa polisi. 

Ofisa
mtendaji mkuu wa Rita, Phillip Saliboko na Meneja masoko na
mawasiliano, Josephat Kimaro wameliambia gazeti la Mwanachi kuwa upekuzi
wa nyaraka zilizotumiwa na Sitti uliofanywa na wanasheria wao, tayari
umekamilika.
“Kazi
yetu (Rita) tumeimaliza na upekuzi wa taarifa za Sitti umekamilika na
kinachofuata sasa ni kupeleka nyaraka hizo kwenye mamlaka inayohusika
ambayo ni polisi, wao ndio wataamua nini cha kufanya,” Kimaro aliliambia
gazeti hilo.
Alisema
Rita haiwezi kumhukumu moja kwa moja mrembo huyo kuwa alighushi nyaraka
na kudanganya ili apate cheti hicho cha kuzaliwa kilichotolewa na Rita
Septemba na badala yake wanapeleka vielelezo walivyonavyo polisi ili nao
wavifanyie kazi.
“Sisi
(Rita) jukumu letu lilikuwa ni upekuzi wa nyaraka, kazi ambayo
imefanywa kwa ustadi mkubwa na jopo la wanasheria wetu na hadi sasa
imekamilika na kinachofuata ni kuzipeleka nyaraka hizo polisi ambao wao
ndiyo wenye jukumu la uchunguzi na kumchukulia hatua Sitti au la,”
alisema.
Sitti
Mtemvu aliingia kwenye kashfa ya kudanganya umri wake na nyaraka zake
mbalimbali zilionyesha alizaliwa 1989, umri ambao umepitiliza ule
unaotakiwa kwa mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania, huku cheti chake
kikionyesha alizaliwa 1991, hivyo kulazimika kuvua taji hilo.
Source: Mwananchi