MOMBASA HALI NI TETE,MSAKO WA POLISI MISIKITINI VIJANA WANNE WAFARIKI
Watu wanne wameuawa kwa kudungwa visu na vijana waliokuwa wamejihami mjini Mombasa Pwani ya Kenya.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/mombasa-hali-ni-tetemsako-wa-polisi.html
Watu
kadhaa pia walijeruhiwa katika shambulio hilo la usiku wa kuamkia leo
kwenye vituo vya basi Kisauni. Bado haijajulikana waliouawa ila
inaaminika walikuwa raia wa kawaida waliokuwa kwenye shughuli zao.
Mwandishi
wa BBC mjini humo Emmanuel Igunza anasema hali ya wasiwasi imetanda
Mombasa huku maafisa wa polisi wakipiga doria mitaani.

Walioshuhudia
mashambulio hayo wanasema vijana waliokuwa wamejihami kwa mapanga na
silaha nyingine butu, waliwavamia watu katika vituo vya magari ya
abiria.
Aidha
inadaiwa vijana hao walikuwa wameziba nyuso zao, wakipeperusha bendera
nyeusi sawa na ile iliyopatikana katika msako wa jana kwenye miskiti ya
Musa na Sakinah, jijini Mombasa.
Awali Polisi walionya kuwa wako tayari kukabiliana na chochote kitakachotokea kufuatia msako huo.
Zaidi ya vijana mia mbili hamsini walikamatwa na silaha kadhaa ikiwemo magurunedi na bastola kupatikana katika misikiti hiyo.
Hata
hivyo viongozi wa Kiislamu na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu
wamelaani msako huo, ambao wanasema utaenndeleza dhana kuwa polisi
wanailenga jamii nzima ya waislamu.
Mwezi Februari, msako sawa na huo uliotekelezwa katika msikiti wa Musa ulisababisha ghasia na kifo cha afisa mmoja wa Polisi.
Chanzo BBC
Chanzo BBC