RONALDO AKANUSHA KUMTUKANA MESSI
Jana Jumanne gazeti la Daily Telegraph l iliandika habari ya kusisimua kutoka kwenye kitabu cha mwandishi wa SKY Sport Guillem Balague...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/ronaldo-akanusha-kumtukana-messi.html
Jana Jumanne gazeti la Daily Telegraph liliandika habari ya kusisimua kutoka kwenye kitabu cha mwandishi wa SKY Sport Guillem Balague kiitwacho “MESSI”.
Katika kitabu hicho Balague ameandika kwamba:
“Ronaldo,
labda ya kwa dalili za kuwa na akili za kitoto ambazo wanazo wacheza
soka wengi, anadhani kwamba kuna ulazima kujitamba mbele ya wachezaji
wenzie, akionyesha hamuogopi Messi na yupo tayari kushindana nae.
“Ndio
maana, kwa mujibu wa baadhi ya wachezaji wa Real Madrid, CR7 amekuwa
akimpa Messi majina ya ajabu kwa kumuita ‘motherf—-r’; na pale
anapomuona mchezaji yoyote wa Real Madrid akiongea na Leo Messi, basi
nae huishia kumuita (tusi) ‘motherf—-r’.”
Taarifa
hii ya Balague ilitengeneza vichwa vya habari vingi kwenye media na
haikumchukua Ronaldo muda mrefu kujibu shutuma hizo kupitia mashabiki
wake millioni 100 kwenye mtandao wa Facebook. Pamoja na kukanusha
taarifa kumtukana Messi – Ronaldo amesisitiza kwamba amewapa wanasheria
wake ruhusa ya kuchukua hatua za kisheria juuya mwandishi huyo, huku
akisema kwamba anawaheshimu wanasoka wote na messi akiwemo
