Mwanamuziki Amin Naye Ajitoa THT Rasmi kama Alivyofanya Linah Sanga
THT jana imemuaga rasmi Amini ambaye miongoni mwa mastar wanaotokea kwenye jumba hilo la vipaji Tanzania baada ya kuishi nd...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/mwanamuziki-amin-naye-ajitoa-tht-rasmi.html
THT
jana imemuaga rasmi Amini ambaye miongoni mwa mastar wanaotokea kwenye
jumba hilo la vipaji Tanzania baada ya kuishi ndani yake kwa zaidi ya
miaka 9 mpaka sasa.
Amini
ambaye anakua msanii wa pili kutoka kwenye uongozi wa THT baada ya
Linah ambaye aliagwa Mwezi July mwaka huu anasema ameishukuru sana THT
kwa muda wote aliokuwa nayo kuanzia kama mwanafunzi hadi baadae kuwa
mwanamuziki kamili.
Baada ya kukamilika kwa
shughuli ya kutoa vyeti kwa walimu na uongozi wa THT akiwemo Mkurugenzi
Ruge Mutahaba,Amini pia aliwapa nafasi waandishi na waalikwa kushuhudia
kipande cha video ya wimbo wake mpya uitwao Mbeleko.
