JOKATE AINGIA STUDIO KUANDAA NGOMA MPYA
Mwanamitindo, mtangazaji wa TV na msanii wa muziki na filamu Jokate Mwegelo ameingia tena ndani ya studio za Pesa Records chini ya pr...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/jokate-aingia-studio-kuandaa-ngoma-mpya.html
Mwanamitindo,
mtangazaji wa TV na msanii wa muziki na filamu Jokate Mwegelo ameingia
tena ndani ya studio za Pesa Records chini ya producer Allonem na
kuandaa wimbo mpya uliopo kwenye hatua za mwisho.

Akizungumza
na Bongo5 hivi karibuni producer wa studio hiyo Allonem, alisema Jokate
amebadilika na kuimba nyimbo za Kiswahili na kudai amebadilika kutoka
kwenye uimbaji wa kutumia Kiingereza zaidi.
“Jokate
tumefanya naye kazi mbili, moja imeshatoka ni ile ambayo ali-perform
kwenye show ya Fiesta Mwanza na baada ya hapo tukakaa chini na kuandaa
wimbo mpya ambapo mpaka sasa hivi upo katika hatua za mwisho,” amesema producer huyo.
“Sema
Jokate sasa hivi yuko mbio sana ila akitulia itamalizika. Pia studio ya
Pesa Record tukiwa chini ya mkurugenzi wetu Mwinyi Pesa tumeanzisha
Pesa Entertainment ambayo ina msanii Becka Title. Atatoa wimbo
ijumaa hii itakuwa kama ndo kama anatuzindulia licha ya kuwa kuna mambo
mengine yatafuata,” aliongeza Allonem ambaye pia alitengeneza beat ya
wimbo wa Fid Q na Bi Kidude.