MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE ATEKWA, AUAWA
SIMANZI! Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Abdu Jumaa iliyopo Kitunda, jijini Dar es Salaam, Enock Mseti (20) a...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/mwanafunzi-wa-kidato-cha-nne-atekwa.html
SIMANZI! Mwanafunzi
wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Abdu Jumaa iliyopo
Kitunda, jijini Dar es Salaam, Enock Mseti (20) alitekwa na watu
wasiojulikana kisha kuuawa kikatili na maiti yake kutupwa kando ya reli
hivi karibuni.
Akizungumza
na gazeti hili nyumbani kwake Kitunda, baba mzazi wa marehemu, Reuben
Mseti alisema kijana wake ambaye hakuwa na tabia ya kushiriki katika
makundi maovu, aliondoka jioni baada ya kufanya kazi zake za nyumbani
kama ilivyokuwa kawaida yake.
“Mwanangu
alikuwa afanye mtihani wa kidato cha nne mwaka huu, ingawa kutokana na
hali yangu kiuchumi kuwa mbaya, alikuwa amesimama kwenda shuleni, lakini
nilikuwa katika jitihada za kuhakikisha anafanya mtihani huo,” alisema
mzee Mseti kwa huzuni.
Jeneza likipelekwa makabulini kwa ajili ya mazishi.
“Hili
ni pigo kubwa sana kwangu na familia yangu ndugu mwandishi, maana
kijana huyu ndiye alikuwa kila kitu hapa nyumbani, ukizingatia mimi na
mke wangu umri umeshatuacha. “Kwa jinsi mwili wake ulivyokutwa,
inaonekana aliuawa mbali na pale alipotupwa kwa sababu katika paji la
uso wake, kulionekana alama ya kupigwa na kitu kizito, mikono na miguu
yake ilikuwa imevunjwa, lakini nguo alizovaa hazikuwa na damu kuonyesha
kama kulikuwa na purukushani.
Mama Enock Mseti(katikati)akiwa mwenye uzuni kubwa.
“Sehemu
aliyokutwa marehemu ni mita chache tu kutoka nyumbani katika eneo
ambalo lina kipori kidogo karibu na ilipopita reli,” alisema mzee Mseti.
Kijana
ambaye ni msaidizi wa kazi za nyumbani kwa mzee huyo aliyejitambulisha
kwa jina la Seleman Abdallah alisema siku ya tukio marehemu aliondoka na
kurudi nyumbani majira ya saa nne kuulizia chakula, akidai kuwa awekewe
kidogo tu kwani asingekula sana, kisha akaondoka.
Baba Enock Mseti kulia akiwa mwenye simanzi kubwa.
“Marehemua
aliondoka na akarudi kama saa 5 hivi usiku na kuondoka tena, lakini
safari hii hakurudi hadi tulipopata taarifa za kufa kwake jambo ambalo
lilitushangaza,” alisema Abdallah. Marehemu alizikwa katika Makaburi ya
Kinyamkera yaliyopo Kitunda jijini Dar es Salaam.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina.
>>>>>>GPL
>>>>>>GPL