MISS TANZANIA MPYA NAYE UTATA MTUPU YADAIWA KUWA SIO MTANZANIA
MISS Tanzania mpya wa 2014, Lilian Kamazima, amesema alihisi ushindi tangu alipoingia katika mashindano hayo, lakini alipokosa ...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/miss-tanzania-mpya-naye-utata-mtupu.html
MISS
Tanzania mpya wa 2014, Lilian Kamazima, amesema alihisi ushindi tangu
alipoingia katika mashindano hayo, lakini alipokosa taji hakuhuzunika
bali alikubali matokeo.
Lakini
zengwe jipya limeibuliwa jana na kuenezwa kwenye mitandao ya kijamii
kwamba Lilian aliyepewa taji hilo baada ya Sitti Mtemvu ambaye ni
mshindi wa awali kujivua taji kutokana tuhuma za kudanganya umri, si
raia wa Tanzania bali ni Mnyarwanda.
Hashim
Lundenga ambaye ni Mkurugenzu wa Miss Tanzania, amekanusha vilivyo na
kusisitiza kuwa ni uzushi kwa sababu wao wanaangalia vyeti vya kuzaliwa
ambavyo vinaonyesha uraia wa mshiriki.
Hayo
yameibuka siku mbili tangu Lilian kukabidhiwa taji la Miss Tanzania
2014, lililokuwa likishikiliwa na Sitti Mtemvu aliyeamua kulivua baada
ya kukumbwa na kashfa mbalimbali tangu kutawazwa kwake Oktoba 11.
Lilian
ambaye awali alikamata nafasi ya pili, alisema: “Sikuwa na kinyongo
ukizingatia urembo ni mambo mengi si sura, ngozi, mwonekano pekee bali
unajumuisha mambo mengi, ndiyo maana kipindi cha usahili huwa kirefu.
Binafsi niliamini kwamba (Sitti) alistahili hasa kutokana na kuwa na
vigezo vingi vinavyoonekana kwa macho hata tulipokuwa kambini,
nilikubali matokeo,” alisema Lilian.
Lilian
alisema kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa kwa matokeo Oktoba 11,
anaamini kilikuwa kigumu kwa Sitti, pia kwake hasa ukizingatia tuhuma
mbalimbali zilizokuwa zikimkabili mrembo huyo aliyetokea katika Kanda ya
Temeke.
“Nina
maono ya mbali na ninatamani miaka mitano ijayo niione Tanzania
iliyokua hasa katika nyanja ya elimu, napenda kuona namba ya wanafunzi
wanaofaulu ikiwa sawa vijijini na mijini ili kuwa na taifa lenye watu
werevu na wenye maendeleo, hivyo nitajitahidi kutumia nafasi yangu
kusongesha gurudumu hili,” alisema.
Mrembo
huyo ambaye kwa sasa yupo nchini Uganda kwa shughuli za masuala ya
mitindo, alisema anafurahia kupata nafasi hiyo na anawaahidi Watanzania
kuwa atafanya kazi kwa nguvu zote ili kuhakikisha anatimiza malengo ya
waandaaji wa mashindano hayo. Lilian Kamazima ana miaka 18, alishiriki
akitokea Mkoa wa Arusha.