MAMBO HADHARANI KUHUSU DIAMOND NA ZARI..!! MAHABA MAZITO
Siku chache baada ya kumwagwa na Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’, Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amenaswa kwenye ma...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/mambo-hadharani-kuhusu-diamond-na-zari.html
Siku
chache baada ya kumwagwa na Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’,
Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amenaswa kwenye mahaba
mazito na msanii, mtangazaji, mjasiriamali, tajiri na mrembo mkali
kuliko wote Afrika Mashariki, Zarinah Hassan a.k.a Zari au Boss Lady.
Mbongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akimhagi msanii mrembo mkali
kuliko wote Afrika Mashariki, Zarinah Hassan a.k.a Zari au Boss Lady.
HABARI YA TAUNI
Habari
ya ‘mujini’ ilidai kwamba, mahaba ya wawili hao yalianzia safarini
walipokutana kwenye ndege moja wiki iliyopita ambapo Diamond alikuwa
akitokea nchini Nigeria kupitia Afrika Kusini kisha Dar huku Zari
akitokea Afrika Kusini kuelekea Dar kibiashara.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, mastaa hao walipokutana kwenye ndege
waliungana na kupiga picha za pamoja kisha safari yao ya mahaba niue
ikaanzia hapo.
UWANJA WA NDEGE
Chanzo
hicho kilimwaga ‘ubuyu’ kwamba, wawili hao walipotua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, Diamond alionekana akiwa ‘veri klozi’ na
Zari kiasi cha kuibua minong’oni uwanjani hapo kwa namna walivyoonekana
wamependezeana.
Diamond Platnumz akipozi na mrembo Zari kimahaba.
KWENYE GARI LA DIAMOND
Ilisemekana
walipofika nje walikwenda moja kwa moja kwenye maegesho ya magari
(parking) kisha walizama kwenye ndinga la staa huyo wa Ngoma ya
Mdogomdogo ambapo waliongozana hadi hotelini.
WENYEJI WA ZARI
“Boss
Lady alifuatwa na wenyeji wake lakini cha kushangaza walishindwa
kumpokea kwani baada ya kumuona yuko kwenye mahaba na Diamond nao
wakajikata kiaina,” alisema sosi wetu.
HOTELINI UFUKWE WA BAHARI YA HINDI
Mtoa
ubuyu wetu huyo aliendelea kunyetisha kwamba, baada ya kutimka airport,
siku ya kwanza walilala hoteli moja maarufu jijini Dar (jina
linahifadhiwa kwa sababu maalum) iliyopo kwenye Ufukwe wa Bahari ya
Hindi.
‘Diamond Platnumz’ akiwa na mrembop huyo kwenye 'pipa'.
WASHTUKIWA, WAHAMA HOTELI
Chanzo
hicho ambacho ni mtu wa karibu wa Diamond au Dangote, kilizidi
kuvujisha kwamba, ilipofika usiku, wawili hao waliamua kuhama kwenye
hoteli hiyo kwa madai kwamba walikuwa wameshtukiwa na watu wengi hivyo
walihofia kunaswa.Ilisemekana kwamba walihamia hoteli nyingine ambayo
nayo ipo pembezoni mwa ufukwe huo.
KOSA LA KIUFUNDI
Katika
harakati zao zote, kosa la kiufundi walilofanya ni kujifotoa wakiwa
kimahaba ufukweni na kuziachia picha hizo kwenye mitandao ya kijamii
huku wakisifiana.
MASHABIKI
Mashabiki
wa jamaa huyo kupitia mitandao hiyo, walidai kwamba huenda Diamond
mwenye umri wa miaka 26, amefanya hivyo ili kumkomoa Wema ambaye
alimtosa Dangote kistaarabu.
Walidai kwamba Zari anaweza kumtangaza zaidi Diamond kimataifa na hasa Uganda tofauti na Wema ambaye angemtangaza Bongo tu.
Mrembo Zari au Boss Lady akiteta jambo.
NENO
“Diamond mjanja sana. Kenya alizua gumzo na msanii Avri na yule demu wa Malindi, Mombasa na baadaye msanii Victoria Kimani.
NIGERIA
“Kule
Nigeria alishakuwa gumzo na akina Davido, Iyanya, Tiwa Savege na Yemi
Alade ambaye walikutana Coke Studio Africa jijini Nairobi, Kenya.
NI ZAMU YA UGANDA
“Ishu
ilikuwa Uganda lakini sasa ni kama ananawa maana ameshapata ‘kiki’
kupitia Zari,” alisema mmoja wa wachambuzi wa habari za mastaa Bongo.
DIAMOND ANASEMAJE?
Baada
ya kunyetishiwa mchongo huo, waandishi wetu walimvutia waya Diamond
asubuhi, mchana, jioni na usiku lakini simu haikupokelewa.Zari ni mzawa
wa nchini Uganda ingawa ana uraia wa Afrika Kusini ambapo anaishi kwa
sasa.
Mkali Zari akiwa na ndinga yake aina ya Black Chrysler (2008).
UTAJIRI WA ZARI
Pamoja
na uzuri wa umbo na sura ikiaminika kuwa ndiye msanii mrembo mkali
Afrika Mashariki, Zari ndiye msanii tajiri wa kike namba moja nchini
Uganda kwa kuwa ana utajiri wa kutisha.
Zari
ana umri wa miaka 32 (anamzidi Diamond kwa miaka 6), akiwa ni mama wa
watoto wawili, aliyeolewa na Ivan Semwanga ambaye mwaka jana ndoa yake
ilidaiwa kuingia mdudu japo haijavunjika, hivyo bado ni mke wa mtu.
Zari
anaingiza mshiko mrefu akimiliki majumba yanayomwingizia fedha ndefu na
magari ya kifahari kama yale ya mastaa wa Kimarekani.
Zari
amepata mafanikio makubwa katika muziki na kipindi chake cha The Boss
Lady kwenye Runinga ya UBC nchini humo, kinachomuingizia mkwanja mrefu
kutokana na matangazo kikifananishwa na kile cha mwanamitindo wa
Marekani, Kim Kardashian cha Keep Up With The Kardashians.
Kwa
mujibu wa Jarida la Times la Uganda, huenda Zari akaingia kwenye orodha
ya wanawake matajiri zaidi Afrika siku chache zijazo endapo ataendelea
kuzichanga.
Aliyekuwa baby wa ‘Diamond Platnumz’, Wema Sepetu akipozi.
MAGARI
Zari
mwenye maskani yake Kampala na Afrika Kusini, anamiliki ndinga kibao za
kisasa na zenye thamani kubwa kama BMW (2006) lenye thamani ya dola
47,000 (Sh. milioni 75.2), Black Chrysler (2008) linalouzwa dola 16,000
(Sh. milioni 25.6) na Audi Q7 (2010) linalogharimu dola 53,000 (Sh.
milioni 84.8).
Mengine
ni Silver Chrysler (2008) lenye thamani ya dola 13,000 (Sh. milioni
20.8), Jetta Volkswagen (2006) linalogharimu dola 27,000 (Sh. milioni
43.2), Mercedes Benz Convertible (2008) linalouzwa dola 26,000 (Sh.
milioni 41.6), Range Rover Sport (2010) lenye thamani ya dola 109,000
(Sh. milioni 174.4), Lamborghini Gallardo (2010) linalogharimu dola
198,000 (Sh. milioni 316.8), Hummer H2 la dola 150,000 (Sh. milioni 240)
na mengine mengi, yote yakiwa na jina lake badala ya namba za usajili.
Pia
Zari anamiliki maduka, hoteli na majumba ya kisasa kwenye miji mikubwa
ya Pretoria na Cape Town nchini Afrika Kusini na Kampala, Uganda. Kazi
ni kwako Diamond!
Source GPL






