MAJANGA; MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI AKUTWA NA HIRIZI DARASANI
MTOTO mmoja wa miaka 9 (jina linahifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Manda iliyopo Kijiji cha Mti...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/majanga-mwanafunzi-wa-darasa-la-pili.html
MTOTO
mmoja wa miaka 9 (jina linahifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa darasa
la pili katika Shule ya Msingi Manda iliyopo Kijiji cha Mtimbira,
wilayani Ulanga, Morogoro wiki iliyopita usiku wa manane anadaiwa
kukutwa darasani akiwa na hirizi kubwa kiunoni.
Tukio hilo lilitokea katika moja ya majengo ya Shule ya Msingi Mazoezi Kigurunyembe ya mjini humo.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililoshuhudiwa pia na mwandishi
wetu, lilijiri Alhamisi iliyopita ambapo mara baada ya kuonekana
darasani humo, baadhi ya wananchi walianza kumpa kichapo wakidai kuwa
yeye ni mwanga.
Dogo
huyo alinusurika kifo kutoka kwa wananchi hao wa Kigurunyembe waliokuwa
na hasira kali baada ya mmoja wa walimu kuwatuliza na kufanikiwa
kumuokoa mwanafunzi huyo na kwenda kumficha kwenye ofisi ya walimu ya
shule hiyo.
Hirizi nyekundu ikiwa kiunoni mwa mtoto huyo.
Akihojiwa na Uwazi mwalimu huyo aliyejitambulishwa kwa jina la Zuhura Khatibu alikuwa na haya ya kusema:
“
Wiki hii mimi ni mwalimu wa zamu nilipofika shuleni nikawashuhudiwa
wananchi wakimshushia kichapo mtoto huyo, kama mzazi niliumia sana
nikawauliza kwa nini wanampiga wakadai eti ni mwanga ameanguka hapa
shule usiku, sisi tulipigwa butwaa. Nilimuoka na kumficha ofisini,”
alisema Zuhura.
Mtoto huyo akiwa na mwalimu wa zamu, Bi. Zuhura Khatibu.
Akizungumza
na mwandishi wetu, mwanafunzi huyo alidai kuwa alitokea Mtimbira kwa
ndege ya kichawi, anatumiwa na wanga na kwamba alipofika pale shuleni
wenzake walimdondosha akaamua kuingia darasani.
Alipoulizwa
alikuwa anaelekea wapi usiku huo, alidai walikuwa wakienda Kihonda kwa
baba yake anayefanya biashara ya mbogamboga. Alipopekuliwa alikutwa na
hirizi kubwa yenye rangi nyekundu kwenye mkanda wa suruali yake,
alipoulizwa ilikuwa ya nini alisema alifungwa ili kumlinda.
Mwalimu Zuhura Khatibu akimpeleka mtoto huyo kituoni.
Baada
ya mahojiano hayo,walimu hao walimkabidhi mwandishi wetu mwanafunzi
huyo ambapo waliongozana na Mwalimu Zuhura hadi Kituo cha Polisi
Morogoro kwenye dawati la jinsia na watoto.
Mkaguzi
Msaidizi wa Polisi wa Dawati la Jinsia na Watoto, Sophia Ngosso
alimpokea mtoto huyo na kufungua taarifa kwenye kitabu cha kumbukumbu
cha polisi jalada namba MOR/RB/12659/014.
Baadaye
iligundulika kuwa mtoto huyo alikuwa anatafutwa na baba yake aitwaye
Clarence Kandira ambaye alifika pale polisi baada ya kupigiwa simu
ambapo alimtambua mwanaye na kuangua kilio na kusema:
Baba wa mtoto huyo kushoto, Clarence Kandira akimshukuru msamaria mwema (Zuhura Khatibu).
“Huyu
mtoto anasoma darasa la pili Mtimbira na ana matatizo ya ugonjwa,
(hakuutaja), tukiwa nyumbani Kihonga alipotea katika mazingira ya
kutatanisha na hii ni mara ya pili, mara ya kwanza alipotea hivihivi na
kuokotwa kwenye Mto Kilombero akiwa ndani ya mtumbwi.”
Alipoulizwa
kwa nini amemfunga hirizi, Kandira alidai kuwa haikuwa hirizi bali ni
alama yake inayomsaidia kuonekana kirahisi anapopotea. Afande Sophia
alimsainisha Kandira na kumkabidhi mtoto wake akaondoka naye.


