HIKI NDO ALICHOKISEMA ZARI KUHUSU ISHU YA KUTOKA KIMAPENZI NA DIAMOND PLATNUMZ.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/hiki-ndo-alichokisema-zari-kuhusu-ishu.html
Mfanyabiashara na mwimbaji mrembo wa
Uganda, Zari the Boss Lady na Diamond Platnumz waliingia kwenye
headlines weekend iliyopita baada ya picha zao wakiwa kwenye faragha
kama wapenzi kuzua maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii.
Hata
Hivyo Zari hakuchukua muda mrefu na kuamua kutumia Instagram kufumbua
fumbo hilo kwa kuweka wazi kuwa ameshirikiana na Diamond katika wimbo
wake mpya.
Zari
ameuambia mtandao wa Big Eye wa Uganda kuwa picha zilizosambaa ni
sehemu ya video shoot ya wimbo aliofanya na hit maker wa Number 1.

Wimbo
huo unatarajiwa kutoka December 18 wakati wa party ya Zari ‘All white
Ciroc party’ itakayofanyika kwenye Club Guvnor nchini Uganda.
Kitu
ambacho watu wengi walikuwa hawafahamu ni kuwa , Zari ni muimbaji
lakini alikuwa ameweka pembeni muziki kwa muda, na sasa ameamua kurejea.
