ZOEZI LA KIJESHI USHIRIKIANO IMARA BURUNDI 2014
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/zoezi-la-kijeshi-ushirikiano-imara.html
Brigedia
Jenerali Joseph Chengelela (kushoto)akimkabidhi bendera ya Afrika
Mashariki msaidizi wa zoezi mara baada ya kukabidhiwa kutoka kwa mgeni
rasmi hayupo pichani siku ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA
2014-BURUNDI.
Meja
Jenerali James Mwakibolwa wa nne kulia akiwa na Brigedia Jenerali
Joseph Chengelela wa tano kulia na Mwambata wa JWTZ nchini Burundi
kanali Venant Mutashobya wa tatu kulia mara baada ya ufunguzi wa zoezi
USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI.

Picha ya Pamoja ya maofisa wa serikali ya Burundi na Maafisa Wakuu wa Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI
Majeshi hayo yakiwa katika mazoezi.
………………………………………………………………………..
Zoezi
la Ushirikiano Imara linalojumuisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
limefunguliwa leo nchini Burundi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa chi
hiyo. Gwaride maalumu linalojumuisha majeshi yote ya nchi wanachama
lilikuwa limesimama mbele ya wageni mbalimbali katika uwanja wa kambi ya
kijeshi ya Muzinga nje ya mji wa Bujumbura wakati Makamu huyo wa Kwanza
wa Rais alipokabidhi Bendera ya jumuiya kuashiria kuanza rasmi wa
mazoezi hayo.
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liliwakilishwa na Meja
Jenerali James Mwakibolwa ambaye ni Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita
Makao Makuu ya Jeshi.
Mazoezi
haya ya medani hufanyika kila mwaka katika moja ya nchi wanachama kwa
utaratibu wa kupokezana yakiwa na lengo kuu la kudumisha ushirikiano
katika masuala ya ulinzi na usalama.
Pamoja
na mambo mengine, mazoezi haya yatatoa fursa kwa nchi wanachama kuandaa
na kuweka mikakati ya pamoja katika kukabiliana na matishio mbalimbali
yanayoweza kutokea katika ukanda wetu wa afrika mashariki.
Maudhui makuu ya zoezi la mwaka huu yanajikita katika kukabiliana na changamoto katika ulinzi wa amani, majanga ya asili na ya kibinadamu, ugaidi, pamoja na uharamia ambavyo vimekuwa tishio katika maeneo mengi duniani.
Aidha, kutakuwa na mazoezi ya kuyaweka tayari majeshi yetu katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ili kupunguza na kuzuia kabisa madhara ya magonjwa hayo.
kwa ujumla, mazoezi haya ni kipimo cha jinsi gani nchi yetu imejiandaa na kujiweka tayari kupambana na changamoto hizi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na jumuiya.
JWTZ limejiadaa vyema katika ushiriki likishirikisha waajeshi wa fai malimali ili kutimiza malengo ya nchi yetu na jumuiya kwa ujumla katika kukabiliana na changamoto zilizotajwa.
Aidha, kikosi cha Tanzania kupitia kitengo cha Uhusiano na Raia (Civil Military Cooperation) kimepanga kutoa misaada mbalimbali kwa wananchi wa Burundi waishio maeneo ya karibu na kambi ikiwa ni pamoja na vifaa kwa ajili ya wanafunzi. Ikumbukwe kuwa, jeshi bora ni lile ambalo askari wake wamefunzwa vizuri na kupata mzoezi ya mara kwa mara katika kutimiza majukumu yao, mazoezi ndiyo hulifaya jeshi letu kuwa tayari wakati wote kuwatumikia wananchi.