Flatnews

LIGI KUU VPL 2014/2015:- YANGA VS SIMBA TAIFA, MBEYA CITY VS AZAM NANI MBABE LEO

Hapo kesho Jumamosi October 18,2014, Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam utarindima kwa Dabi ya Kariakoo wakati Vigogo wa Soka N...



Hapo kesho Jumamosi October 18,2014, Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam utarindima kwa Dabi ya Kariakoo wakati Vigogo wa Soka Nchini Tanzania na Watani wa Jadi, Yanga SC na Simba SC, watakapovaana katika pambano lao la kwanza la Ligi Kuu Vodacom kwa Msimu wa 2014/15.


Watani hao wanatinga kwenye kimbembe hiki kinachongojewa Nchi nzima hasa kwa vile Msimu huu kila Timu ina Benchi la Ufundi jipya kwa Yanga kuwa na Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania kutoka Brazil Marcio Maximo, na Simba kuongozwa na Kocha wao wa zamani Mzambia Patrick Phiri.
Vile vile mvuto zaidi ni ule wa kuona Wabrazil wa Yanga SC, Kiungo Andrey Ferreira Coutinho na Geilson Santos ' Jaja' wakivaana na Simba SC iliyomteka Straika wa Yanga, Mganda Emmanuel Okwi.

Hii itakuwa Mechi ya 4 ya Ligi kwa kila Timu lakini Yanga SC wanaingia wakiwa Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 6 wakati Simba SC wako Nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 3.

Msimu huu, Yanga SC walianza kwa kuchapwa 2-0 na Mtibwa Sugar huko Morogoro na kisha kushinda Mechi mbili mfululizo dhidi ya Ruvu JKT na Prisons, zote kwa Bao 2-1 kila moja.

Simba SC wao hawajafungwa lakini hawajashinda hata Mechi moja katika Mechi 3 walizocheza kwa kutoka Sare na 2-2 na Coastal Union na Sare za 1-1 dhidi ya Stand United na Polisi Morogoro.

Refa wa mtanange huu wa Jumamosi ni Israel Nkongo ambae atasaidiwa na Ferdinand Chacha na John Kanyenye wakati Hashim Abdallah atakuwa Refa wa Akiba na Kamishna ni Salum Kikwamba.

Msimu uliopita, Refa Israel Nkongo ndie aliesimamia Mechi ya Mahasimu hawa ambapo Yanga SC waliongoza 3-0 hadi Mapumziko na Simba SC kuweza kurudisha na kupata Sare ya 3-3.


Nao Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Azam FC watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Mbeya City ambao hawajafungwa hata goli moja msimu huu wakati  timu hizo zitakapovaana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya keshokutwa.

Azam FC ambao mpaka sasa wamecheza mechi 37 za Ligi bila kufungwa ikiwa Nane za msimu wa 2012/13, 26 za msimu uliopita 2013/2014 na tatu za msimu huu 2014/2015, watashuka kwenye uwanja huo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi mgumu wa 2-1 dhidi ya ‘wababe’ hao, ushindi ambao uliwapa Ubingwa wa VPL Machi 23,mwaka jana wakiwa mechi moja mkononi.

Post a Comment

emo-but-icon

item