Umeshawahi kuiona Helcopter ya Mchungaji Gwajima hii hapa
Ni miezi kadha sasa tangu ulipozuka uvumi wa Mchungaji Kiongozi na Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kununua He...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/umeshawahi-kuiona-helcopter-ya.html
Ni
miezi kadha sasa tangu ulipozuka uvumi wa Mchungaji Kiongozi na Askofu
wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kununua Helcopter.
Kanisa la hilo limeitambulisha rasmi picha ya helcopter hiyo kupitia
ukurasa wake wa facebook. Kwa mujibu wa Mch. Gwajima, Helcopter hiyo
aina ya Robinson 44 itatumika kuhubiri injili katika mikoa mbalimbali
nchini.
Pamoja na Hayo, Mchungaji huyo amesema kuwa kama kila kitu kitakwenda sawa; Helcopter itazinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda. Tayari usajili wa Chopper hiyo umekamilika na kupewa nambari za usajili 5H-OLY.
Pamoja na uwepo wa Helcopter hiyo; Mchungaji Gwajima pia amesema
anatarajia mwakani kupokea ndege nyingine tatu; na tayari amepata kibali
cha kujenga uwanja wa ndege ujenzi ambao utaanza mwishoni mwa mwaka
huu.
>>>>JF