Cuba yatuma madaktari zaidi kutibu Ebola
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/cuba-yatuma-madaktari-zaidi-kutibu-ebola.html

Rais
wa zamani wa Cuba, Fidel Castro, anasema nchi yake itatuma karibu
madaktari na wauguzi 300 zaidi kusaidia kupambana na Ebola Afrika.
Alisema Cuba iko tayari kushirikiana na Marekani kwa masilahi ya amani duniani.
Cuba imeshatuma madaktari na wauguzi 165 huko Afrika Magharibi.
Katika
tukio jengine, Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa ripoti yake
ya siri iliyofichuliwa nje ya shirika, ambayo ilidai kuwa shirika hilo
lilifanya makosa katika kushughulikia janga hilo la Ebola, haikuwa
kamilifu na ilikuwa bado haikuchambuliwa.
WHO imesema uchambuzi kamili wa hatua ilizochukua utakamilika baada ya ugonjwa wa Ebola kudhibitiwa.