Flatnews

UALIMU NGAZI YA CHETI WAFUTWA


Waziri   wa  Elimu  na Mafunzo ya ufundi,  Dkt Shukuru Kawambwa
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi, Dkt Shukuru Kawambwa.
Serikali   kupitia  Waziri   wa  Elimu  na Mafunzo ya ufundi,  Dkt Shukuru Kawambwa  imefuta mafunzo ya ualimu  ngazi  ya cheti kuanzia mwaka huu ili kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini.
Akizungumza na Wanafunzi  wa  Chuo cha Ualimu Tabora Dkt  Kawambwa amesema kuanzia mwaka huu serikali imeyafuta mafunzo  ya ualimu ngazi ya cheti  ikiwa ni   mkakati  maalumu wa kuboresha kiwango  cha  elimu  hapa  nchini.
Amesisitiza kuwa Walimu watakao   ajiriwa   kufundisha  shule za msingi  na   sekondari watatakiwa kuwa  na  elimu  ya  kiwango cha diploma na  kuendelea. Kuanzia sasa Wizara yake imejipanga kusimamia   ubora  wa  elimu ndio maana  imeamua kuanzisha   utaratibu huo  mpya.
Katika  hatua   nyingine   kuanzia  mwaka   huu   walimu   ambao  wataajiriwa  kufundisha shule ya msingi  na   sekondari   ni  lazima  wawe   na   elimu  ya  kiwango  cha Diploma na wasiofikia kiwango  hicho   watapewa  fulsa ya kujiendeleza.

Post a Comment

emo-but-icon

item