Flatnews

KATAVI KUYASHUGHULIKIA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE ?

Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe .


Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe .
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe .
Mkoa wa Katavi  kupitia  mpango  wa Taifa  wa chanjo  na  wadau  mbalimbali  utaendesha  kampeni  shirikishi ya  chanjo  dhidi  ya Surua Rubella, matone ya vitamin A, utoaji wa  dawa za minyoo na kinga dhidi  ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele.
Akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari   Dkt Rajabu Rutengwe  ameeleza kuwa katika kampeni  hiyo chanjo ya  surua-rubella itatolewa kwa watoto wote wenye umri kati ya miezi tisa hadi miaka mitano.
Matone ya Vitamini A  yatatolewa  kwa watoto wenye umri kati ya miezi sita na miaka mitano, dawa dhidi  ya minyoo itatolewa kwa watoto wenye umri kati ya mwaka mmoja na miaka mitano, kinga tiba dhidi ya matende, mabusha au ngiri maji na usubi kwa wenye umri wa miaka mitano na kuendelea.
Kampeni ya Chanjo ya surua inaendeshwa ikiwa ni muendelezo wa utaratibu wa kufanya kampeni kila baada ya miaka mitatu, utaratibu huu unaotokana na ukweli kwamba baadhi ya watoto hukosa chanjo ya surua  katika utaratibu wa kawaida.
Katika hatua hatua nyingine   watoto 15 kati ya 100 wanaopewa chanjo ya surua hawajijengei kinga ya mwili ya dhidi ya surua, hali ambayo  husababisha kutokea  milipuko ya surua.

Post a Comment

emo-but-icon

item