Matebele wapenda ngono na wavivu–Grace Mugabe
Dr Grace Mugabe na Mumewe Rais Robert
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/matebele-wapenda-ngono-na-wavivugrace.html

Mke wa
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe Grace Mugabe siku hizi ni dokta, cheo
kilichozua mtafaruku nchini mwake akikinzwa katika udaktari wake wa
masuala ya sosholojia alioupatia katika chuo kikuu cha nchi hiyo,
amewatemea cheche wanaume wa eneo la Matabeleland nchini humo kuwa ni
hodari wa kuoa wake wengi kila uchao na kuwazalisha watoto na kushindwa
kuendeleza makazi yao .
Dokta
Mugabe aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara unaokisiwa kuhudhuriwa
na watu wapatao elfu nne katika viwanja vya Gwanda mapema wiki hii.
Dokta Mugabe amewashangaa wanaume hao kutoka kabila la Ndebele kwa kuwa
maarufu wa kuzalisha na kuwatelekeza watoto bila matunzo yoyote huku
wakiendekeza ngono Zaidi.BBC
Dr Grace anasema ni jambo la kawaida kumkuta mwanamume ana wake watano hadi kumi na kuuita ni upuuzi mkubwa.
Pmaoja na
hayo ,Dr Mugabe amewashutumu pia wanaume hao wa Matabele kusini kwa
kushindwa kufanya maendeleo yao binafsi na badala yake mawazo yao ni
kusafiri kuelekea Africa Kusini hasa katika jiji la Johannesburg kufanya
kazi za nyumbani.
Hii ni
mara ya pili katika kipindi cha miaka miwili familia ya Mugabe kuwakosoa
wanaume wa Matebele hadharani kwa kukimbilia Africa Kusini kuajiriwa
kama watumishi wa ndani.
Mara ya
kwanza alikua ni Rais Mugabe aliyezua mjadala mkali kutoka kwa watu wa
Matebele, ambapo alitoa kauli kama za mkewe katika eneo hilo hilo mwaka
wa jana.Dr Grace Mugabe pia amewashutumu wanaume wa eneo hilo kwa
ubakaji na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.
Pamoja na
kuwatemea cheche hizo Dokta Grace Mugabe alishangazwa na umati mkubwa
uliojitokeza kumlaki katika mkutano huo , huku wakimpigia makofi
mazito,akiwemo waziri wa michezo na utamaduni Andrew Langa,mwenyekiti wa
ZANU PF Simon Khaya Moyo na waziri Abdenico Ncube.