MAHABA NIUE YAMFICHA SNURA 'MAMAA MAJANGA'
MAHABAT! Kuonesha kwamba mahaba yamemkolea, staa wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’ amedaiwa kukacha shughuli za muziki...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/mahaba-niue-yamficha-snura-mamaa-majanga.html
MAHABAT! Kuonesha
kwamba mahaba yamemkolea, staa wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Mamaa
Majanga’ amedaiwa kukacha shughuli za muziki na kutumikia penzi lake kwa
mahaba motomoto.

Kudhihirisha
hilo, chanzo chetu kimevujisha picha za mrembo huyo akiwa na mchumba
wake anayefahamika kwa jina moja la DJ Hunter wakiwa katika malovee
mazito kwa kupigana mabusu.
“Yani Snura sasa hivi muziki ameuweka pembeni anatumikia mahabati mwanzo mwisho,” kilidokeza chanzo chetu.

Meneja wa Snura, Mohamed Kavu ‘HK’.
Jitihada za kumpata msanii huyo kuzungumzia ukimya wake kwenye gemu hazikuzaa matunda lakini meneja wake, Mohamed Kavu ‘HK’ amekuwa
akisisitiza kuwa msanii wake huyo yupo nchini Afrika Kusini katika
shughuli za kimuziki huku pia kukiwa na madai kuwa msanii huyo ni
mjamzito tarifa ambazo pia zinakanusha na HK.