YAJUE MAKOSA MATATU MAKUBWA DIAMOND ALIYOWAKOSEA WATANZANIA HADI WANAMZOMEA NA KUMCHUKIA….
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/yajue-makosa-matatu-makubwa-diamond.html
Katika
pitapita zangu Instagram nkakutana na picha na maneno yaliyoandikwa na
mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Bikira Wa Kisukuma. Baada ya kusoma
nkasema sio mbaya kama ntashea kilichoandikwa na Bikira kwa wasomaji
wangu . Hebu soma na kisha tupe maoni yako je ni kweli kua Diamond
kafanya makosa haya??????
“DIAMOND ANA MAKOSA 3 MAKUBWA ALIYOTUTENDEA WATANZANIA:
1.Kosa
la kwanza ni KUWA NA BIDII KWENYE MUZIKI WAKE…Hili ni kosa kubwa sana
kwa Watanzania..Hakupaswa kuwa na bidii hivi..Angekuwa tu wa KAWAIDA
kama wenzake waliopita ili AFULIE awaachie na wengine waje kwenye chati
arudi Tandale kuuza Wali..
2.Kosa
la 2 ni KUJITAMBUA YEYE NI NANI..Kwanini ajitambue wakati wenzie wenye
majina walishindwa??Kwani yeye nani awe tofauti??Hii ni DHARAU KUBWA
sana kwa Watanzania na Wanamuziki wenzie na inaonyesha ana
KIBURI..Diamond kujua yeye ni Mwanamuziki mahiri na kutumia VALUE yake
aliyoipata kwa mbinde kuiletea sifa Tanzania nje ya Mipaka ni KOSA
KUBWA!
3.Kosa
lake la 3 ni KUUHESHIMU MNO MUZIKI UNAOMPA HELA…Kwanini asiwe kama
wakina Mr nanihii tu,kwani wao hawakuhit kama yeye?Mbona waliishi
kawaida tu na kuuchukulia muziki poa hadi walipofulia na leo hata
wakiingia Masai Club nobody cares..Kwani kufulia kitu gani?Diamond
hakupaswa kuuheshimu Muziki kama kazi..Angefanya bora liende tu aimbe
imbe yaishe..Sasa kujifanya Anatoa Collabo mara Davido mara Mafikizolo
mara Trey Songs na K’Cee na Yemi Alade AMETUMWA NA NANI??Huku ni
kutafuta sifa tu alipaswa awe mdogo milele awaachie na wenzie.. Kwa
makosa haya ma3 WATANZANIA wameamua kumuadhibu..Diamond Anaringa…Ana
dharau sana..Anaupenda sana Muziki uliompa JINA..HESHIMA..PESA..na
ametafutiwa REPLACEMENT kwa sababu tu ANAHESHIMU MUZIKI KAMA KAZI na sio JUST SINGING FOR FAME…Watanzania
tumeamua kuadhibu MTU ANAYEHESHIMU KAZI YAKE iliyomtoa from Zero to
Hero na tutamshusha kwa lazima taji apewe mwingine..Watanzania tunataka
Diamond awe another Mr Nice ili tupate kitu cha KUCOMPARE…Shida yetu kuu
wala sio dharau ila ni KWANINI DAI HASHUKI???? Hardwork Pays! Respect
Pays! Knowing Your Value Pays! Kama alimpandisha MUNGU…Hakuna wa kumtoa
pale… Nasibu..wakomeshe..Toa ule wimbo na MAFIKIZOLO wiki ijayo tuone
kama watazomea Spika za redio zao…
