CRISTIANO RONALDO AFUNGA BAO LA 70 LIGI YA ULAYA, REAL IKIIUA LIVERPOOL 3-0 ANFIELD
Liverpool FC 0 -3 Real Madrid All Goals... by soccerpremium
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/cristiano-ronaldo-afunga-bao-la-70-ligi.html
Liverpool FC 0 -3 Real Madrid All Goals... by soccerpremium
Mshambulizi hatari na mwanasoka bora wa dunia, Mreno Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la 70 katika michuano ya mabingwa Ulaya, huku Mfaransa Karim Benzema akifunga mara mbili na kuwazamisha ‘ vigogo wa England’ Liverpool kwa mabao 3-0 katika uwanja wa Anfield. Real Madrid walifunga manao yote hayo katika muda wa dakika 41 za kipindi cha kwanza na kujichimbia kileleni mwa kundi B kwa asilimia 100.
Real ilizifunga FC Basle na Ludogorets Razorad katika michezo miwili ya mwanzo ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa pili katika uwanja wa ugenini na mabingwa hao watetezi wanahitaji pointi moja tu ili kufuzu kwa hatua ya mtoano. Katika mchezo dhidi ya Liverpool usiku wa jana, Real ilishambulia mno na kutawala mchezo.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers bado haelewi kilichomkuta mshambulizi wake Mario Balotelli ambaye amekosa makali, Rodgers alimtoa mchezaji huyo mara baada ya mapumziko na kumuingiza uwanjani kiungo-mshambulizi, Adam Lallana ambaye alionyesha uhai katika kipindi cha pili akicheza na kijana, Rahem Sterling. Kiungo chipukizi wa Ujerumani, Emre Can , 20 aliingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Jordan Herndason, pia Rodhers alimuingiza uwanjani kinda Lazar Markovic dakic, 20 dakika hiyo hiyo na mabadiliko hayo yaliisaidia Liverpool ambao walionekana kubadilika na kucheza mpira katika kipindi cha pili.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, ulimalizika kwa wenyeji, Ludogorets kuichapa Basle kwa bao 1-0 hivyo kufanya timu hizo kulingana pointi na Liverpool na zote zina nafasi ya kufuzu kwa hatua ya pili.