KURA YA HAPANA YAMPONZA, MWANASHERIA MPYA AAPISHWA RASMI ZANZIBAR
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/kura-ya-hapana-yamponza-mwanasheria.html

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein
akimuapisha Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika
hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Mwanasheria huyo ameteuliwa na Rais chini ya kifungu cha sheria namba 55 (1) cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Uteuzi huo umefanyika oktoba 7 mwaka 2014 ambapo Bw. Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasherian Mkuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Katika hatua nyingine Bw Hassan Said anachukua nafasi ya aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Zanziba Bw Othman Masoud ambaye uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa vifungu vya 53, 54(1) na 55 (3) vya katiba ya ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kifungu 12(3) cha sheria ya utumishi wa umma Namba 2 ya 2011.
Kufutwa kazi mwanasheria mkuu wa Zanzibar kunatokana na kupiga kura ya hapana katika vifungu mbalimbali vya katiba iliyopendekezwa Bungeni mjini Dodoma wiki kadhaa zilizopita.