BBA Hotshots: Washiriki wa Kenya, Uganda, na Nigeria watolewa mchezoni, Laveda aponea chupuchupu
Mtanzania Laveda Jumapili October 19 aliponea chupuchupu kwa kubaki kwenye jumba la Big Brother Africa, huku akiwashuhudia washiriki...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/bba-hotshots-washiriki-wa-kenya-uganda.html
Mtanzania
Laveda Jumapili October 19 aliponea chupuchupu kwa kubaki kwenye jumba
la Big Brother Africa, huku akiwashuhudia washiriki wenzake watatu wa
kike wakitoka mchezoni.
Sabina, Lilian, Esther
Esther
(Uganda) , Lilian (Nigeria) pamoja na Sabina (Kenya) ndio washiriki
walioondolewa katika shindano hilo usiku wa jana ikiwa ni ‘eviction’ ya
pili toka shindano lianze.
Hadi
sasa washiriki watano wa kike wametoka katika shindano hilo na kufanya
idadi ya washiriki wa jinsia ya kike kubaki 8 huku wanaume wakiwa 13.
Nchi
za Zambia, Mozambique, Kenya, Uganda and Nigeria kila moja imeshapoteza
muwakilishi mmoja hivyo zote zimebaki na muwakilishi mmoja mmoja tu
mjengoni.
