DK. CHENI: RUSHWA YA NGONO WANAITAKA WENYEWE!
KASHFA! Staa wa filamu za Kibongo, Muhsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amekanusha tabia ya wasanii wakubwa kuwaomba rushwa ya ngono wasanii ...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/dk-cheni-rushwa-ya-ngono-wanaitaka.html
KASHFA! Staa
wa filamu za Kibongo, Muhsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amekanusha tabia ya
wasanii wakubwa kuwaomba rushwa ya ngono wasanii chipukizi na kudai
wanaziendekeza wao wenyewe.
Akipiga
stori na paparazi wetu, Dk. Cheni alisema yeye hajawahi kumuomba msanii
rushwa ya ngono, isipokuwa anaamini walio wengi huanzisha mahusiano
yaliyo rasmi kwa makubaliano yao kutokana na hisia zinavyowasukuma.
“Sizani
kama ni rushwa ya ngono, naamini wengi wanakubaliana, sehemu ya watu
wengi mnapokutana inatokea watu kupendana na kuwa wapenzi hilo nakubali
sababu ni jambo la kawaida hata wasanii kwa wasanii kupendana, sidhani
kama mtu anaweza kulazimishwa kufanya mapenzi ili acheze filamu, mpaka
watu kufanya tendo hilo wameshakubaliana,” alisema Dk. Cheni.
