Visa vya mapenzi haviishi…. huyu wa Dodoma kamuua mke kwa rungu, chanzo?
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/visa-vya-mapenzi-haviishi-huyu-wa.html
Siku
hizi mapenzi yamekua kama karata hivyo kila mmoja anacheza ajuavyo au
awezavyo kwenye huu uwanja mpana ambao kwa kiasi kikubwa miaka
inavyosogea ndio vifo vingi hutokea kutokana tu na visa vya mapenzi.
Taarifa
kutoka Dodoma na kuthibitishwa na Polisi, zinahusu Wananchi kupatwa na
hasira na kumuua Mwanaume aliyemuua mke wake kwa kumpiga na rungu
tumboni kwenye kijiji cha Mzogole.
Mwanamke
aliyeuwawa ana umri wa miaka 48 Mwajuma Chomola na mume wake ambae ndio
mtuhumiwa ana umri wa miaka 55 anaitwa Richard Kodi ambapo kwa mujibu
wa gazeti la HabariLEO, Mwanaume huyu alifariki dunia wakati akihudumiwa hospitali ya wilaya ya Mpwapwa.
Wakati
uchunguzi ukiendelea, matokeo ya awali yanaonyesha chanzo cha yeye
kumuua mke wake waliekua wakiishi pamoja ni wivu wa kimapenzi na kwamba
ishu ilianzia pale Mwanamke alipochelewa kurudi nyumbani akitokea kwenye
sherehe iliyofanyika kwenye kijiji hichohicho wanachoishi lakini mume
alidhani mke kaenda kwengine.
Yaani
sio kwamba alimfumania bali alihisi tu mke wake kaenda kwengine ndio
sababu iliyomfanya akachukua haya maamuzi, mara nyingi kwenye mapenzi
kumekua na kesi nyingi zinazosababisha Wanawake kupigwa au kuuwawa kwa
sababu tu Mwanaume anahisi vitu kama hivi bila kuwa na ushahidi.