Maajabu ya Dunia: Anamkodisha Mpenzi wake ili Apate pesa ya Kununua iPhone 6
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/maajabu-ya-dunia-anamkodisha-mpenzi.html
Mwanafunzi
wa Chuo kikuu kimoja cha China ambaye jina lake halikutambulika kwa
haraka ameamua kufanya kioja ili mradi tu aipate pesa ya kununua aina
mpya ya iPhone iliyoingia sokoni, iPhone6.
Kijana huyo wa alionekana
akiwa nje ya chuo kikuu cha Songijiang akiwa na bango kubwa
lililoandikwa kwa kichina na kutafsiriwa ‘Girlfriend Sharing’.
Katika tangazo hilo
kijana huyo anaeleza kuwa yuko tayari kumkodisha mpenzi wake kwa mtu
yeyote atakayeweza kutoa pesa ili jamaa apate kiasi cha kutosha kuinunua
iPhone 6 yenye screen kubwa.
Picha ya kijana huyo imesambaa kwa kasi katika mtandao wa kijamii unaotumiwa na wachina uitwao ‘Weibo’ ambao ni kama Twitter.
Tangazo hilo limeambatana
na picha za mpenzi wake na amewatoa hofu wateja wanaosita kuingia nae
mkataba kuwa hata mpenzi wake ameridhia na yuko tayari kudate na mtu
yeyote atakaejitokeza.
Muda wa kuwa na msichana
huyo baada ya kumkodi umebainishwa kutokana na malipo yatakayofanywa na
mteja. Viwango ni vya saa 1 (10 yuan), siku 1 (50 yuan) au mwezi mmoja
(500 yuan).
Hata hivyo, wapenzi hawa
sio wa kwanza kujiweka sokoni ili wapate bidhaa ya kampuni ya Apple.
Mwaka jana katika uzinduzi wa iPhone 5, wanandoa wa Shaghai waliwaweka
sokoni watoto wao watatu ili wapate pesa ya kununua computer na simu za
iphones lakini walikamatwa na kufunguliwa mashitaka.
Lakini pia kijana mdogo wa Hunan alijitolea kuuza figo lake ili apate pesa ya kununua iPad na iPhone.
Siyo hayo tu, hivi
karibuni mwanaume mmoja wa Saudi Arabia ametaka kupewa iPhone 6 kama
mahari ya dada yake hata kabla aina hiyo ya simu haijazinduliwa Bahrain.
CREDIT: TIMES FM TZ.
