UNAAMBIWA HIVI NDIVYO MADEE ALIVYOENYESHWA NA POLISI BAAADA YA KUTUUMIWA KUTEKA
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ hivi karibuni alilala katika Kituo cha Polisi cha Kigambon...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/unaambiwa-hivi-ndivyo-madee.html
Msanii
wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ hivi
karibuni alilala katika Kituo cha Polisi cha Kigamboni, Dar akihusishwa
na utekaji wa dereva wa bodaboda, Suedi Waziri (pichani) kisha kumpa
kipigo ambapo inadaiwa alisoteshwa kinomanoma.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ akiwa mikononi mwa Polisi.
Baada ya tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, Ijumaa lilinasa picha zinazomuonyesha msanii huyo akihenyeshwa kituoni hapo huku mmoja wa watu wanaoishi karibu na eneo hilo akinyetisha kuwa, licha ya ustaa wake Madee alikiona cha mtemakuni.
Dereva wa bodaboda, Suedi Waziri aliyetekwa na kushambuliwa na Madee.
“Mimi nilikuwepo pale kituoni, nilimshuhudia akiwa amepigwa pingu huku polisi kama sita hivi, mmoja akiwa na silaha wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi wakimpeleka mahakamani.“Alionekana aliyechoka sana huku akiwa na hofu ila inavyodaiwa baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wakihaha kumnusuru baada ya kulala selo,” kilidai chanzo hicho.
Majeraha ya mguuni aliyopata Suedi Waziri baada ya kushambuliwa na Madee.
Kufuatia msala huo, msanii huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kigamboni na baadaye kuwekewa dhamana na baba yake ambapo kesi yake itatajwa tena Oktoba 6, mwaka huu.
Madee anadaiwa kumteka Suedi na kwenda kumsulubu nyumbani kwake Manzese baada ya kijana aliyekuwa amepakia kwenye bodaboda yake kukwapua simu ya msanii huyo na kukimbia.
Katika kushinikiza simu yake irudishwe ndipo Madee alipomtaiti Suedi na mwisho wa siku akaishia mikononi mwa polisi kwa kufunguliwa kesi iliyosomeka: VJB/RB/625/2014 KUTEKWA KWA BINADAMU
Imeandikwa na Mayasa Mariwata, Shani Ramadhani na Rhoda Josiah.
>>>>GPL