KUWA NAYE KWASABABU NI MCHEZAJI WA AJABU KWETU”-RODGERS
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/kuwa-naye-kwasababu-ni-mchezaji-wa.html
Brendan Rodgers ana matumaini kuwa Daniel Sturridge anaweza kurudi mechi ya watani wa jadi
KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers hajakata tamaa kuhusu Daniel Sturridge kucheza kwa dakika chache kwenye mechi ya watani wa jadi wa Merseyside kesho dhidi ya Everton.
Liverpool imemkosa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England tangu alipopata majeruhi ya mguu akiwa katika majukumu ya kimataifa mapema mwezi huu, lakini sasa anakaribia kurudi uwanjani.
Wakati huu akikosekana kikosini, kikosi cha Rodgers kilipoteza mechi dhidi ya Aston Villa na West Ham, walishinda ligi ya mabingwa dhidi ya Ludogorets na walisubiri kusonga mbele kwa penalti dhidi ya Middlesbrough katika michuano ya Capital One Cup.
Sturridge akitembea uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Aston Villa katika dimba la Anfield.
“Tutafurahi kuwa naye tena na tunatumaini inaweza kuwa wikiendi hii,” alisema kocha huyo.
Sturridge bado hajawa fiti kwa mechi baada ya kuumia katika majukumu ya timu ya taifa ya England, lakini Rodgers anasema ana nafasi ya kuanzia benchi didi ya majirani zao na mahasimu wao, Everton.
“Hayuko fiti kwa ajili ya mechi, hajacheza kwa wiki kadhaa, lakini itakuwa jambo kubwa kuwa naye kwasababu ni mchezaji wa ajabu kwetu”