TUACHE KUIGA MAMBO YASIO NA MSINGI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/tuache-kuiga-mambo-yasio-na-msingi.html
Wazima ndugu na marafiki, kama kawaida…kila siku hua kuna jambo linalowekwa mezani na kuanza kuzungumziwa. Leo nimekuja na mada muhimu sana ingawa watu wengi hulipuuzia….tabia ya kupenda kuchunguza nani anafanya nini, au anaishije imekuwa kero hasa kwa jamii zetu. Sio vijana wala wazee wamekuwa na tabia za umbea umbea…oh mama fulani kanunua gari gani, au kaongeza nini nyumbani kwake….wewe inakuhusu nini….kama sio tamaa na chuki ilijaa moyoni mwako.
Unakuta vijana ndo kabisaa tena haswa vyuoni hupenda kuchunguzana maisha ya wenzao….ndio maana mwisho wa siku huishia kuharibika na kupotea njia ili tuu alijilinganishe na mtu fulani. Kama wewe huna uwezo wa kununua nguo au kubadilisha style ya nywele kila wiki…kwanini usitulie na kuridhika na hali ya maisha uliyonayo….mpaka ukajifananishe na mtu fulani ili iweje…..unajikuta unaanza biashara ya kuuza mwili wako ili tuu upate hela ya kununua hivyo vitu. Maradhi mengi sikuizi na hii dunia ya leo iliyojaa magonjwa na anasa…., vijana tunazidi angamia kwa kuendekeza vitu visivyo na msingi.
Hii ni kitokana na kupenda kuiga kila kitu tunachokiona kwenye televisheni au nchi za nje , tunajikuta tunaiga hata vitu ambavyo sio utamaduni wetu, kwa mfano mavazi yaliyoacha sehemu kubwa ya mwili wazi, vyakula mbalimbali na hata mitindo ya nywele na uchezaji wa miziki fulani fulani. Jamani imefika muda sasa tubadilike na kuongezee juhudi na nguvu kazi katika kujenga taifa letu. Na sio kuendekeza au kujikita katika mambo yanayopotosha jamii na hata vizazi vya baadae.
Kila mtu akijitambua na kufanya vitu vyenye kufundisha na kuonya jamii, hakika tutakuwa mahali pazuri baada ya miaka kadhaa hapo mbeleni.Tusiwe watu wa kuiga kila kitu tunachokiona kwa watu, vingine vibaya.Unakuta kisa msanii fulani amevaa nguo fulani na kupaka vipodozi fulani ma wewe unaiga….na ngozi yako kama kenge….kwanza si kila fashion inampendeza mtu….inategemea na umbile lako…ohoo utaishia kuchekwa na watu barabarani kisa tuu na wewe uonekane umevaa nguo hiyo.
Mimi kama kijana mwenzenu, ningependa kutoa ushauri tuu katika jamii yangu, kwamba mambo yako na vitu vyako viendelee kuwa vyako, penda kuwa wewe na sio kama mtu fulani , kuwa kielelezo katika jamii yako….na vivyo hivyo usipende kufatilia mambo ya watu kwani daima yatakurudisha nyuma….kama unataka maendeleo, jifunze kwa walioweza…na waliofanikiwa.
Kama mdau na mwananchi jaribu kutoa maoni au ushauri na eleza ni chanzo haswa cha vijana wa sikuizi kuaribikiwa kwa kufata mambo yasiyokua na maadili katika jamii yetu….ili tuzidi kueleweshana zaidi….ltiririka hapo chini….kuwa mzalendo na uonyeshe upendo kama unajali…..ni hayo tu.
Chanzo: Bealicious
