'Si Lazima Kujua Kingereza Kwani Mie Muingereza, Hata Messi Hajui' - Ray
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/si-lazima-kujua-kingereza-kwani-mie.html
Mkurugenzi
wa Kampuni ya filamu Rj Company,Vicenti Kigosi amesema si lazima kujua
Kingereza maana hata Messi hajui, Ray amesema hayo alipokuwa akichat
Live na mashabiki zake kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika
kipengele cha Kikaangoni Live
SI LAZIMA NIJUE KIINGEREZAMkali huyo ambae kwa sasa anachukuliwa kama moja ya watu wenye mafanikio
katika tasnia ya filamu nchini ambae pia ameshawishi vijana kibao
kuingia katika tasnia hiyo amefunguka na kuweka wazi kuwa suala la lugha
ya kiingereza kwake ni changamoto lakini si jambo la ajabu sabgabu kuna
watu wengi maarufu duniani wanapigwa chenga na lugha ya kiingereza.Prince Dully >>>>Mbona haujui kingereza au uliishia darasa la saba,nini?RAY Kigosi >>>>>>Hata messi hajui kiingereza kwani mimi muingereza nijue Kiingereza.CHUCHU MCHUMBA WANGUMsanii Vicent Kigosi ambae katika hizi siku za karibuni ilisikika kuwa
yupo katika mahusiano na msanii mwingine wa filamu ambae anafahamika
kama Chuchu Hansi hivyo ilipelekea mashabiki wa ukurasa wa facebook wa
EATV kutaka kujua ukweli juu ya mahusiano hayo na kama kweli jamaa
anampango wa kumuoa binti huyo au laah,na majibu ya Ray uyalikuwa kwamba
wawe watulivu muda utakapofika ndio watajua ukweli wote juu ya suala
hilo.
kinachokukutanisha na watu mahiri kila siku ya jumatano kuanzia saa sita za mchana mpaka nane kamili.
