PICHA; KIPA THIBAUT COURTOIS AMEONGEZA MIAKA MITANO TENA NDANI CHELSEA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/picha-kipa-thibaut-courtois-ameongeza.html
KIPA bwana mdogo wa Chelsea Thibaut
Courtois ambaye kwasasa ndiye chaguo la kwanza la kocha Jose Mourinho, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano.
Hatua hiyo inazidi kumweka pabaya kipa Petr Cech ambaye kwa miaka kumi iliyopita alikuwa kipa namba moja.
Courtois
ameanza kuichezea Chelsea msimu huu licha ya kusajiliwa tangu mwaka
2011 ambapo alilazimika kupelekwa Atletico Madrid kwa
mkopo ili kuongeza uzoefu.
Courtois
akaicheza kwa mafanikio Atletico Madrid kwa misimu mitatu mfululizo
baada ya kujiunga na Chelsea kutoka Genk ya nyumbani
kwao Ubelgiji.
Akarejea Stamford Bridge msimu huu na
kucheza
mechi yake ya kwanza dhidi Burnley na kuisadia Chelsea kuibuka na
ushindi wa 3-1 na baada ya hapo akamsugulisha benchi Petr Cech
mechi zote zilizofuata.
Sasa Cech, 32 atalazimika kuangalia
uwezekano wa kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine pindi utakapowadia msimu wa usajili wa dirisha dogo la mwezi Januari.
Taarifa
iliyotolewa kupitia mtandao rasmi wa Chelsea imesema: “Chelsea Football
Club ina furaha kutangaza kuwa Thibaut Courtois, 22 amesaini mkataba
mpya wa miaka mitano.”
