Mchungaji Ampiga Chini mke wa Kwanza na Kuamua Kuoa wa Pili "Dogodogo": Soma Zaidi Hapa
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/mchungaji-ampiga-chini-mke-wa-kwanza-na.html
Kwa
mujibu wa chanzo, ndoa hiyo ilifungishwa na Askofu Innocent Lugagi wa
Kanisa la White House la Durban, Afrika Kusini, Agosti 29, mwaka huu.
Mke
mwingine wa mtumishi huyo wa Mungu anaitwa Zuwena (Catherine) aliyemuoa
mwaka 1985. Lakini kuna madai kwamba, mke huyo amemwacha.
Chanzo
chetu ndani ya kanisa hilo kilidai kwamba, mchungaji huyo aliwaambia
waumini wake aliamua kumuoa Pamela kwa vile ndoa yake ya mwanzo
aliifunga akiwa Muislam na alifungishwa na shehe (hakumtaja jina).
“Alituambia Mungu amemfunulia na amempa mke mwingine mwema ambaye ni binti mbichi, watu wewee,” kilisema chanzo.
Habari
zaidi zinasema kuwa, mchungaji huyo baada ya kutua nchini, Jumapili
moja akiwa kanisani kwake aliwatangazia waumini wake, hasa wanaume
kwamba kama wana wake ambao walichukuana wakati wa ‘ujinga’ na wamekaa
nao kwa miaka mitatu au zaidi na hawana tabia ya Kimungu, mkorofi na
mchokozi na hawajafunga nao ndoa, wawaache ili Mungu awape wake wema.
Sasa baada ya picha za mtumishi huyo kusambaa hadi kwenye mitandao, Risasi , juzi lilifika kanisani kwake Mbezi ili kuzungumza naye lakini hakuwepo.
Sasa baada ya picha za mtumishi huyo kusambaa hadi kwenye mitandao, Risasi , juzi lilifika kanisani kwake Mbezi ili kuzungumza naye lakini hakuwepo.
Baadhi
ya waumini walioweza kuzungumza na Risasi walionesha kushtushwa na
kitendo cha mchungaji wao kumuoa Pamela lakini hawakuwa tayari kusema
neno!
Baadaye mwandishi wetu alimtafuta mchungaji huyo kwa njia ya simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
Baadaye mwandishi wetu alimtafuta mchungaji huyo kwa njia ya simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nipo Kiluvya kikazi lakini hilo lipo ila ni jambo langu binafsi siyo la kulitangaza.”
Baadaye alimtumia ujumbe mwandishi akiwa ameuandika hivi:
“Sanchawa mimi ni Nabii wa Mungu Yehova, uliponipigia tu kila kitu Mungu akaniambia nia yako na kusudi lako.”
Baadaye alimtumia ujumbe mwandishi akiwa ameuandika hivi:
“Sanchawa mimi ni Nabii wa Mungu Yehova, uliponipigia tu kila kitu Mungu akaniambia nia yako na kusudi lako.”
Pia
Risasi lilizungumza na baadhi ya wachungaji wa makanisa ya kiroho
Tanzania ili kuwasikia wanasemaje kuhusu kitendo cha mtumishi huyo
kufunga ndoa nyingine.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao, baadhi ya wachungaji hao walimpongeza Mchungaji Peter kwamba, aliona alikokuwa na anakokwenda ndiyo maana aliamua kuchukua uamuzi huo.
Credit: Harun Sanchwar- Risasi/Gpl